Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bi. Monica Mwamunyange
akibadilishana kadi na Profesa Liu Xueyi kutoka Chuo kikuu cha Southwest
Jiatong, wakati mkufunzi huyo na wanafunzi wa chuo hicho walipotembelea
wizara ya Uchukuzi leo mchana kujifunza na kubadilishana uzoefu katika
masuala ya reli hasa reli ya mwendo kasi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bi Monica Mwamunyange, akifafanua
jambo kwa Wakufunzi na wanafunzi wanaochukua shahada za Uzamili na
Uzamivu katika Reli kutoka Chuo Kikuu cha Southwest Jiatong, wakati
walipotembelea Wizarani hapo kujifunza na kubadilishana uzoefu hasa
kwenye usafiri wa Reli, leo mchana.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bi Monica Mwamunyange (wa nne kutoka
kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi, wanafunzi na sehemu
ya wakurugenzi wa Wizara ya Uchukuzi, wakati wanafunzi hao wanaochukua
shahada za uzamili na uzamivu katika Eneo la Reli kutoka chuo kikuu cha
Southewest Jiatong walipotembelea Wizarani hapo leo mchana ili
kubadilishana uzoefu hasa katika treni za mwendo kasi. Aidha chuo hicho
kimeahidi kubadilishana uzoefu na Chuo che Reli Tabora ili kujenga uwezo
katika masuala ya Reli. (Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi)



No comments:
Post a Comment