BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwatangazia watu
wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi,Mei 2015 kama
Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kilianza rasmi tarehe 1
Julai, 2014 hadi tarehe 30 Septemba, 2014 kwa ada ya Shilingi 50,000/=. Aidha kuanzia tarehe 1 Oktoba, 2014 hadi
tarehe 31 Oktoba, 2014 waombaji watajisajili kwa ada ya Shilingi 65,000/- (ada
pamoja na faini).Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema
kwa njia ya mtandao kupitia
tovuti ya
Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz Kabla ya kujisajili kwenye mtandao,
waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mtihani kuchukua namba rejea
(reference number) zinazotolewa bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta
au M-pesa.
Imetolewa Na:
Kaimu Katibu Mtendaji
Baraza la Mitihani la Tanzania.

No comments:
Post a Comment