Social Icons

Tuesday, 24 June 2014

Benki ya Barclays yatoa somo la ajira kwa wanafunzi wa UDBS

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

01
Meneja Rasilimali Watu wa Benki ya Barclays Tanzania, Anna Chacha (kulia) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS) jana kuhusu fursa mbalimbali za ajira ndani ya benki hiyo na pia nini wafanye ili kuweza kumudu ushindani katika soko la ajira ndani ya sekta za kibenki.
 
02
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Neema-Rose Singo (kushoto) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS) jana kuhusu fursa mbalimbali za ajira ndani ya benki hiyo na pia nini wafanye ili kuweza kumudu ushindani katika soko la ajira ndani ya sekta za kibenki.
03
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Barclays Tanzania, James Meitaron (kulia) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS) jana.
04
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS) wakishiriki semina  kuhusu fursa mbalimbali za ajira iliyoandaliwa na Benki  ya Barclays Tanzania chuoni hapo, Dar es Salaam jana. Mbali na fursa zilizo ndani ya benki hiyo pia walielekezwa nini wafanye ili waweze kumudu ushindani katika soko la ajira ndani ya sekta za kibenki.
05
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya Barclays Tanzania, Khalifa Gwando (kulia), akipokea barua za wasifu (cv) kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS) jana mara baada ya semina kuhusu fursa mbalimbali za ajira ndani ya benki hiyo na pia nini wafanye ili kuweza kumudu ushindani katika soko la ajira ndani ya sekta za kibenki.

No comments: