Social Icons

Monday 5 May 2014

CHUO KIKUU CHA DODOMA CHAFANYA BONANZA, LAFANA


Ndugu wanavyuo na Taasisi mbalimbali za Elimu ukiwa na tukio lolote tutumie kupitia blogzamikoa@live.com
Mwalilishi wa PPF Kanda ya Kati Ndugu Julius S Shayo akimkaribisha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof.Idrissa Kitila (kulia) wakati wa kufunga tamasha la michezo Boanza la wiki moja lililo kuwa limefadhiliwa na mfuko huo.
Pror.Idrissa Kikikagua kikosi cha timu ya Sayansi asilia na Hesabu.
Kikosi kamili cha timu ya Sayansi asilia na Hesabu(ndani ya jezi nyeupe) kikiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Kikosi cha timu ya Sayansi Jamii kikiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha Shule ya Sayansi ya mawasiliano na Elimu Angavu kikiwa katika jezi ya blue na mgeni rasimi.
Washindi wa pete kikosi cha Elimu. Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii Kanda ya Kati Dodoma.

*************
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM,Prof.Idrissa Kitila mwishoni mwa wiki alifunga BONANZA la michezo mbalimbali iliyofanyika chuoni hapo kwa muda wa wiki moja.Michezo hiyo ilifadhiliwa na mfuko wa mafao ya Jamii PPF ambapo ilikutanisha timu mbali mbali katika mpira wa pete na mguu.

Timu zilizoshiriki zilikuwa nane,timu kutoka School saba na timu kutoka Utawala moja.Pamoja na mpira wa Pete na Miguu kulikuwepo mashindano ya kuvuta kamba na kukimbiza kuku,Katika siku ya kufunga mashindano hayo.

Mfuko wa hifadhi ya jamii PPFwaliwakilishwa na Bwana Julius S.Shayo mwakilishi wa kanda ya kati. Katika bonanza hilo ambalo pamoja na kufadhili walitoa mbali mbali ikiwamo vikombe kwa washindi pamoja na fedha taslimu.

Washindi katika Mpira wa miguu amao fainali zilikutana timu kutoka Shule(School)ya Sayansi Asilia na Hesabu na Chuo cha Sayansi Jamii washindi walikuwa Sayansi Asilia ambao walivalia Jezi nyeupe walipata ushindi wa goli sita kwa goli tano.

Kwa upande wa Mpira wa Pete Ulio kutanisha timu za Shule(School) Elimu na Shule Sayansi Jamii na Elimu Angavu Washindi walikuwa Shule ya Elimu kwa jumla ya vikapu 26 kwa 16.

No comments: