Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dkt. Shukuru Kawambwa.
Na Mwandishi Wetu
Katika
kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika sekta ya Elimu,
Serikali itawazawadia wanafunzi na shule zilizofanya vyema katika
mitihani ya Elimu ya msingi na Sekondari.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam Jumatatu April 14, 2014 na Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dkt. Shukuru Kawambwa alipozungumzia
na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Wiki ya Elimu.
Kwa
mujibu wa Dkt. Kawambwa, maadhimisho ya wiki hiyo ya Elimu itakayoanza
Mei 3 hadi 9 mwaka huu ni ya kwanza nchini na yanalenga katika kutambua
juhudi za kuendeleza ubora wa Elimu nchini.
“Pamoja
na malengo mengine, wiki hii italenga katika kutoa motisha na zawadi
kwa shule na wanafunzi waliofanya vizuri ikiwa ni utekelezaji wa wa
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa,” alisema Waziri Kawambwa.
Miongoni
mwa malengo ya BRN katika kukuza ubora wa elimu nchini ni pamoja na
kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi wa shule zinazoonekana kuvuka
viwango vya kukuza ubora.
Kwa
mujibu wa Dkt. Kawambwa, maadhimisho hayo yatakayofanyika mjini Dodoma
yatazinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda pia yatafungwa na Rais
Jakaya Kikwete.
Kwa mujibu wa Waziri Kawambwa, maadhimisho hayo yataanzia katika ngazi ya Wilaya, Mikoa na kasha kufanyika Kitaifa.
Alisema viongozi wote wa Mikoa na Wilaya wamekwishapewa taarifa ya kufanya maandalizi hayo ili kufanikisha sherehe hizo.
BRN
ni Mpango wa utekelezaji wa miradi mikubwa chini ya Ofisi ya Rais
ukilenga kuhakikisha kuwa miradi iliyopewa kipaumbele inapewa fedha za
kutosha ili kupata maendeleo ya haraka
No comments:
Post a Comment