Social Icons

Thursday 27 March 2014

TAARIFA: SERIKALI YAFUTA VYUO 9 VISIVYO NA SIFA.


SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imekunjua makucha yake kwa kutangaza kuvifuta vyuo 10 ambavyo havikusajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Naibu Waziri wa wizara hiyo, Philip Mulugo, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaama mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuongeza kuwa kufutwa kwa vyuo hivyo ni kutokana na kutokufuata utaratibu wa kusajiliwa.

Alivitaja vyuo hivyo ni Media and Research Center, Vision Hotel and Tourism College, East Africa College of Hospitality and Tourism, The Africa Institute of Business Management na Aspiration Training Center, vyote vya Dar es Salaam.

Vingine ni Dar es Salaam School of Hair Design, Media and Values Training Institute na Information Technology Training Center vya Dar es Salaam. Pia alikitaja Chuo cha Morogoro School of Medical Sciences cha Morogoro.

No comments: