Jumla
ya Walimu wapya 36,021 ambao wamehitimu mwaka 2013 kutoka vyuo
mbalimbali hapa nchini wataajiriwa rasmi na Mamlaka za Serikali za Mitaa
(Halmashauri) ifikapo tarehe 01 Aprili 2014. Kati ya idadi hiyo walimu
wa ngazi ya Cheti (Daraja III A) ambao hufundisha katika shule za Msingi
ni 17,928 na walimu wa shule za sekondari ni 18,093 (wakiwemo 5,416 wa
Stashahada na 12,677 wenye shahada).
Orodha
rasmi ya walimu wapya ikionesha Halmashauri mbalimbali walikopangwa
itatangazwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) ifikapo tarehe 15 Machi, 2014.
Walimu
wote wapya wanatakiwa kuripoti bila kukosa kwenye Halmashauri
walikopangiwa ifikapo tarehe 01 Aprili, 2014 ili waanze kazi mara moja.
Inasisitizwa
kwamba walimu waripoti tarehe hiyo ili taarifa zao za kiutumishi
zifanyiwe kazi na Waajiri wao yaani Wakurugenzi ili kuwawezesha kupata
mshahara mwezi Aprili 2014 na hivyo kuepuka ulimbikizaji wa mshahara kwa
watumishi wapya wanaoanza ajira.
Mwalimu
yoyote ambaye ataripoti baada ya tarehe 10 Aprili, 2014 bila sababu za
msingi zinazokubalika kiutumishi atakuwa amepoteza nafasi hiyo.
Ikumbukwe
kwamba Upangaji wa Walimu wapya kwenye Halmashauri umezingatia uwepo wa
mahitaji ya walimu. Vile vile, fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba
na nauli ambazo zitalipwa kwa kila mwalimu atakayeripoti kulingana na
viwango vilivyowekwa na Serikali zimetumwa kwenye Halmashauri
walikopangwa walimu hao. Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kwenda kuripoti
katika Halmashauri alikopangwa.
Ofisi
ya Waziri Mkuu TAMISEMI haitafanya mabadiliko yoyote ya vituo vya
kufanya kazi walimu wapya isipokuwa kwa utaratibu wa kawaida wa uhamisho
baada ya mwalimu kutimiza vigezo na masharti ya uhamisho.
Ni
vema ifahamike kuwa ajira zinazotangazwa ni za walimu wapya. Walimu
ambao tayari ni watumishi umma waliokuwa vyuoni kwa ajili ya
kujiendeleza kielimu na hivi sasa wamehitimu mafunzo yao, wanatakiwa
kurudi kwa waajiri wao na kuendelea na kazi.
IMETOLEWA NA
JUMANNE A. SAGINI
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI
No comments:
Post a Comment