Tovuti ya Times Fm imefanya mahojiano ‘exclusively’ na Robina Nicholaus,
msichana aliyeshika nafasi ya kwanza/ aliyeongoza kitaifa (Tanzania
One) kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2013.
Robina, mwenyeji wa wilaya ya Bunda mkoa wa Mara ambaye alikuwa anasoma
katika shule ya wasichana ya Marian, akiwa na ndoto ya kuwa daktari wa
watoto amejibu maswali kumi muhimu na majibu yake yanaweza kuchukuliwa
kama mfano wa kuigwa kwa wanafunzi walioko shuleni ambao wanakumbwa na
changamoto kadhaa, na wazazi wanaowapeleka watoto wao shule.
Ulifanya nini ghafla ulipopata taarifa kuwa umekuwa wa kwanza Tanzania nzima, na je, ulitegemea?
Nilipopata matokeo kwamba nimekuwa wa kwanza, kwanza nilifurahi sana na
kilichobaki zaidi ilikuwa ni kumshukuru Mungu kwa sababu yeye ndiye
kayawezesha yote. Nilihisi kama kupaa vile…nilifurahi sana halafu my mom
alikuwa pale… alikuwa analia akaniinfluence na mimi machozi yatoke, I
was very happy yaani. Sikutegemea kuwa wa kwanza lakini nilikua na
uhakika wa kufanya vizuri kwa sababu niliplan kufanya vizuri.
Kama msichana ulifanya nini kuzivuka changamoto za kimasomo na kufanikisha kwa kiasi kikubwa?
Safari ya taaluma ni ndefu ndio, kwenye safari ya masomo kuna changamoto
za hapa na pale, ambapo mara nyingi wasichana waga tunafanya maamuzi
ambayo sio sahihi. Lakini kwangu mimi nimeweka interest yangu sana kwa
wazazi. Kwa hiyo nilikuwa open kwa wazazi na kuwaomba ushauri wa hapa na
pale nifanye nini. Na katika vyote nilivyokuwa nafanya ni kufanya kile
kitu ambacho hakiwezi kusubiria kwanza ambacho ni masomo. Kwa hiyo
naweka juhudi pale ili ukishafanya kila mtu ajue kwamba umefanya.
Ilikuwa mbaya sana kwenye kusoma hasa form three ambapo nilianza kushuka
and all that. Kwa hiyo wazazi pamoja na walimu pia walikaa na kuweza
kunisaidia na mimi mwenyewe nilikuwa tayari kusikia ushauri wao na
kuweza kusoma kwa bidii zaidi ili niweze kupata ile nafasi yangu
niliyokuwa naipata toka nianze.
Nini kilichofanya ushuke kimasomo wakati huo?
Kilichofanya nishuke ni ile kupoteza malengo na juhudi zangu, na pia
kuona kwamba vitu vinaanza kuwa vigumu halafu kuweka hiyo kwenye akili
kwamba hicho ni kigumu siwezi kukifanya. Lakini nilipoamua kuweka juhudi
na kuona kwamba ni vitu vya kawaida kwamba navyozidi kukua na vitu
vinazidi kuwa vigumu na natakiwa nitafute njia ya kuvi-overcome, ndo
hivyo nikaweza kufanikiwa.
Ratiba yako ya siku ulipokuwa shule kwa ujumla wake ilikuwa vipi na muda gani ulikuwa unajisomea?
Asubuhi nilikuwa naamka mapema kabla ya time table ya shule haijaanza
kwa sababu tunatakiwa tuamke mapema kwenda misa kwenye saa kumi na moja
hivi. Kwa hiyo naamkaga kwenye saa tisa najiandaa naenda darasani kwa
sababu siwezi kusoma usiku kwa sababu usiku nakuwa nimechoka, kwa hiyo
my extra time inakuwa asubuhi ambako I’m still fresh.
Nasoma then ikifika muda wa misa naenda kusali. Nikitoka kusali kuna
kazi ndogo ndogo za kufanya kujiandaa na time table ya school and all
that. And my free time ile mchana nikitoka darasani kuanzia saa nane,
nakuwa nimepanga nini
natakiwa nifanye, ni somo gani natakiwa kulisoma at that time ambapo ni
saa nane mpaka saa kumi na nusu. Ambapo ni muda wa concentration, kama
kuna kitu ambacho sijaelewa naenda kuwafuata waalimu kwa sababu wanakuwa
wapo at that time. And kuna some free time
kama ile break time, ni kuanzia saa nne na dakika 40 mpaka saa tano na
robo, pale hauwezi kusema unatake breakfast all the time, unatake
breakfast for a short time halafu nyingine inabaki unaweza kufanya
maswali matano ya physics. Yaani every little time ambayo unaweza
kuipata, you don’t let it go to waste tu, una-utilize.
Marafiki ulionao wanaweza kusaidia kukupandisha au kukushusha. Wewe ulikuwa na marafiki wa aina gani?
Marafiki wangu nimewachagua kwa category..yeah (anacheka), ikifika muda
wa kusoma nakuwa na mtu ambaye najua atanisaidia, kwa hiyo nilikuwa na
rafiki yangu anaitwa Sarafina amekuwa wa nne. Alikuwa ananiinfluence sana kusoma, huyo ni wakati wa kusoma, kwenye academics namfata yeye.
Ikifika wakati wa social siwezi kumfata sarafina kwa sababu she is not
that social, yeye yuko kama mimi we are not that social, kwa hiyo ninaye
social friend. Pia ikifika
muda wa kuspend, I have an economical friend. Ambaye I’m sure nikikaa
nae nikiwa naspend siwezi kwenda beyond my budget. Kwamba siwezi
kufulia. Kwamba we are all in the same status, same friends, yeah.
Ni kitu gani kilikuwa kinakuboa sana shuleni na kukunyima furaha muda mwingine?
Kitu ambacho kilikuwa kinaniboa sana, ikifika wakati ambapo kwa mfano
watu wachache kwenye darasa wamefanya kosa halafu sasa mnakuwa included
as a whole class halafu mnapata adhabu. Hiyo adhabu directly itaharibu
time table yangu ya kusoma. Kwa hiyo badala ya kusoma nafikiria
ningekuwa nasoma physics, I’m either slashing an area..yaani hiyo
ilikuwa inaniboa sana yaani.
Ulishawahi kuitwa ‘Msongo’ au majina kama hayo? Ulikuwa unaichukuliaje na je, ilikutenga na marafiki zako?
Yeah, msongo…kauzu. Yeah mimi naipenda hivyo kwa sababu nafanya
nachotakiwa kufanya ambacho ni kusoma. Hiyo haikunitenganisha na
marafiki zangu.
Vuta taswira, je, ingetokea ukapata division Zero na kuwa wa mwisho Tanzania nzima ungefanyaje? Na unawashauri nini waliofeli kwa kiasi hicho?
Kama ningepata zero, kwanza ningefikiria…na ningekuwa very disappointed
kweli, lakini pia ningefikiria kuhusu kujipa second chance, ningeenda
kusoma tena.
Kwa waliofeli ningependa kuwashauri wasikate tamaa hata kidogo and wajipe second chance. Kwa wengine pia ambao wana vipaji vyao wanaweza kuviendeleza. But pia kwa kuwa elimu ni muhimu..ku-reseat pia ingekuwa ana option.
Robina Nicholaus ni msichana wa aina gani?
Robina ni mtu mkimya lakini mcheshi pia. Nisingependa nikae na mtu
halafu nikawa kimya just because ni mkimya... I will try kuchekesha, and
of course I’m funny anyway.
Chanzo Times Fm
No comments:
Post a Comment