Social Icons

Saturday 15 February 2014

SOMA HAPA: NAFASI ZA KAZI KUTOKA UHAMIAJI


Kamishna Mkuu wa idara ya Uhamiaji anatangaza nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji kwenye

vyeo vya Koplo na Konstebo wa uhamiaji.

A: MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI NAFASI 70
1. SIFAZINAZOHITAJIKA
Awe na shahada ya kwanza au Stashahada ya juu kutooka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na serikali katika fani zifuatazo; Sheria, Uchumi, Biashara, Utawala, Uandishi wa habari, Ualimu, Usafirishaji, Rasilimali watu, Sayansi ya kompyuta, Teknolojia ya mawasiliano, Takwimu, Uchapaji, Uhandisi majengo na Uhandisi Mitambo.
Awe na umri usiozidi miaka 35
2. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
(i) Kusimamia doria sehemu za mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini.
(ii) Kusimamia shughuli za upelelezi, kuandaa hati ya mashitaka na kuendesha mashitaka.

(iii) Kutoa na kupokea fomu mbali mbali za maombi ya hati za uhamiaji
(iv) kufanya ukaguzi wa mwanzo wa maombi mbalimbali
(v) kupokea na kukagua hati za safari, fomu ya kuingia na kutoka nchini.
(vi) kuidhinisha malipo mbalimbali ya huduma za uhamiaji kwa wanaostahili
(vii) kuagiza ufunguaji wa majalada ya watumiaji
(viii) kutunza kumbukumbu za ruhusa kwa wanaongia na kutoka nchini
(ix) kukusanya, kusimamia na kutunza takwimu za uhamiaji na uraia
(x) Kuandaa majibu ya maombi yote ya huduma za uhamiaji yaliyokubaliwa au kukataliwa ZINAENDELEA


B. KOPLO WA UHAMIAJI (NAFASI 100)


1. SIFA ZINAZOHITAJIKA
(i) Awe amehitimu Kidato cha Sita na kufaulu
(ii) Awe na umri usiozidi miaka 30


C. KONSTEBO WA UHAMIAJI (NAFASI 100)


1. SIFA ZINAZOHITAJIKA
(i) Awe amehitimu kidato cha nne na kufaulu
(ii) Awe na umri usiozidi miaka 25


D. SIFA ZA ZIADA: KOPLO/KONSTEBO WA UHAMIAJI
(i) Cheti cha ufundi stadi (Full Technical Certificate) kwenye fani ya umeme na mitambo.
(iii) Cheti au Stashahada ya Uhazili (Certificate or Diploma in Secretarial Studies)
katika chuo kinachotambulika na Serikalì.
(iv) Cheti au Stashahada ya Takwimu (Certificate or Diploma in Statistics) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
(v) Cheti au Stashahadayavyombo vya Majini (Certificate or Diploma in Marine Transportation
and Operation) kutoka katika Chuo kinachotambulika na Serikali.
(vi) Cheti au Stashada katika fani ya uchapaji (Printing)
(vii) Ujuzi na elimu ya kompyuta na uandishi mzuri utazingatiwa.


E. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
(i) Kufungua, kupanga na kutunza majalada yenye orodha ya majina ya watumiaji wa huduma
za Uhamiaji.
(ii) Kuandika Hati mbalímbaLi za Ubamiaji
(iii) Kufanya Doria schcme za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, treni na sehemu zenye
vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwcmo vya majini.
(iv) Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za Uhamiaji Mahakamani pamoja na wageni
wanaofukuzwa nchini (Deporters).
Kufanya ukaguzi kwcnye mahoteli, nyumba za kulaLa wageni na sehemu za biashara.
(vi) Kuchapa au kuandika kwa kompyuta barua au nyaraka mbalimbali zinazohusu kazi za kila
siku za Uhamiaji.
(vii)Kufanya matengenezo/ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya Uhamiaji.


F: MAOMBI YOTE YAWE NA VIAMBATANISHO VIFUATAVYO. 
(i) Vivuli vya vyeti vya kumalizia masonia kwa mujibu wa sifa zilizotajwa.
(ii) Nakala ya Cheti cha Kumaliza Elimu ya Msingi
(iii) Nakala ya cheti cha kuzaliwa
(iv) Picha mbili (passport size)
(v) Barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa.


G: UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yapite posta na barua za maombi ziandikwe kwa mkono.


(i) Maombi ya nafasi ya mkaguzi msaidizi wa uhamiaji yatumwe kwa;


KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
S.L.P 9223,
DAR ES SALAAM


(ii) Maombi ya nafasi ya Koplo wa uhamiaji na konstebo wa uhamiaji yatumwe kwa;


KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI,
S.L.P 512,
DAR ES SALAAM

No comments: