Social Icons

Tuesday 28 January 2014

ASKARI 96 WA TANAPA WAMALIZA MAFUNZO YA AWALI WAAHIDI KUPAMBANA NA MAJANGILI‏



Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan kijazi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya kuhifadhi maliasili katika chuo cha wanyama pori cha Mlele mkoani katavi ambao hawapo pichani hapo juzi katika chuo cha wanyama pori cha mlele ambapo wahitimu 96 walihitimu mafunzo ya awali ya wahifadhi wa rasilimali za nchi na aliwataka wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa ili waweze kupambana na kutokomeza ujangiri na kuvunja mitandao ya majangiri ya ndani ya nchi na nje ya nchi.
 Askari wa hifadhi ya  mbuga ya wanyama (TANAPA)  wakiwa wamesimama wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA  ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu
 
 Askari wa hifadhi ya  mbuga ya wanyama (TANAPA) wakiwa wamekaa wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ALLAN KIJAZI ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu.
 Picha na Katavi yetu Blog

*********************
Na   Walter Mguluchuma wa Katavi yetu Blog.
Mpanda Katavi
 Jumla ya  Askari 96 wa  Shirika  la Hifadhi la Taifa  la Wanyama Pori  (TANAPA) wametimu    mafunzo  ya miezi   mitatu  katika  chuo     kipya   cha wanyama   pori   cha Mlele  kilichopo   Mkoa  wa Katavi  na kutoa  kiapo cha utii  mbele ya Mkurugenzi mkuu  wa TANAPA Allan Kijazi

Askari hao  wa TANAPA walimaliza  mafunzo  hayo  hapo juzi  kwenye chuo  hicho   cha  wanyama Pori  cha Mlele  akiwa ni  mafunzo ya  kwanza  hapa  nchini  kwa TANAPA  kutoa  mafunzo kama hayo kwa Askari wa wanyama pori kupatiwa mafunzo hayo  kabla ya kuanza  kazi

Katika  Risala yao ya  wahitimu wa mafunzo hayo  ya kulinda maliasili  iliyosomwa  na Bruno  Mbunda  walieleza kuwa wamejifundisha  mbinu mbalimbali za kulinda   rasilimali za Taifa  kwa Vitendo   na nadharia

Waliyataja baadhi ya mafunzo waliyoyapata kuwa ni namna ya kufanya doria , kukamata  waharifu  kumpekua  mharifu  na kutotumia  nguvu  sana  katika kukamata  mharifu    pamoja  na  pia wamejifundisha namna ya kutumia silaha

Walieleza  katika kipindi hicho cha  mafunzo    wahitimi   hao walifanikiwa kukamata  waharifu  hamsini  wakati  wakifanya  doria  katika maeneo mbambali ya Mbuga ya  Katavi  na kwenye mapori ya akiba ya Rukwa  Lwafi

Wahitimu hao walieleza kuwa  mafunzo hayo yaliwashirikisha  Askari  99  lakini  watatu kati yao wameshindwa  kuhitimu  zikiwemo  sababu  mbambali  kama  utoro na utovu  wa nidhamu   hari ambayo ilfanya wahitimu  waliomaliza kubaki  96 ambapo kati yao mwanamke  ni mmoja  na wanaume ni  95

Kwa upande wake mkuu wamapori ya akiba  ya  Rukwa Lwafi  Joseph Mbung’ombe alimweleza mkurugenzi mkuu wa TANAPA kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa mawasiliano  na  ubovu wa miundo  mbinu ya barabaa  na  upungufu  wa  magari pamoja  idadi ndogo ya washiriki  wa mafunzo kwa wanawake na ufinyu  wa bajeti

Nae  Mkurugenzi  wa Hifadhi  na Ikolojia  Martini  Loibook  alieleza kuwa mafunzo hayo walioyapata yanaumuhimu  sana  hasa kutokana na changamoto  zinazoikabili nchi  yetu  inayokabiliwa na wimbi la ujangili

Pia Mkurugenzi wa  utumishi   na utawalla   wa TANAPA  Witnes Shoo  aliwataka wahitimu hao  kufanya kazi  kwa uaminifu  kwa kujituma  na  wawe na didamu  na  wasiwe na tabia ya kutow a siri za ofisi

Mkurugenzi Mkuu   wa TANAPA  Allan Kijazi  aliwaasa wahitimu hao  wahakikishe wanafanya kazi  zao kwa uaminifu mkubwa  hasa  katika shughuli zao  katika kupambana kukomesha ujangili
Aliwataka kutojihusisha  na masuala ya ujangiri na badal awahakikishe wanafanya kazi za kupambana na mitandao ya ujangiri iliyopo ndani ya nchi na nje ya nchi

Alisema wapo baadhi ya watumishi wa TANAPA ambao wamekuwa sio waaminifu hivyo wahitimu hao wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu pasipo kueubuniwa na mtu yoyote yule au watu

No comments: