Social Icons

Monday 16 December 2013

BASI LA CHAMPION LAPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI 29 KATIKA MLIMA CHIMWAGA LIKITOKEA CHUO KIKUU DODOMA (UDOM)


Gari lenye namba za usajili T 704 ADR  aina ya Scania bus la kampuni ya CHAMPION.
Gari lenye namba za usajili T 704 ADR  aina ya Scania bus la kampuni ya CHAMPION lillokuwa likiendeshwa na dereva ALLY RAMADHANI, mnyaturu, umri kati ya  35 - 40, mkazi wa Kisasa Dodoma likiwa limebeba wanamichezo/wanavyuo wa vyuo vikuu vya Zanzibar na State University Zanzibar likitokea chuo kikuu Dodoma (UDOM) likielekea kituo kikuu cha mabasi Dodoma lilipinduka na kusababisha majeraha kwa abiria wapatao 43 kati yao Majeruhi  29   waliotibiwa na kuruhusiwa  na majeruhi 14 wamelazwa katika Hospitali ya  Rufaa ya Mkoa Dodoma, wote wakiwa ni wanaume.




Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kamishna msaidizi wa Polisi SUZAN S. KAGANDA amesema ajali hiyo imetokea tarehe 15/12/2013 majira ya saa 06:15 hrs huko eneo la mlima wa Chimwaga UDOM         Kata ya  Makulu Dodoma mjini.

Kamanda KAGANDA amewataja majeruhi katika ajali hiyo ambao ni:-

1. Hamisi Hamisi, miaka 28, mshirazi, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 1.
2. Bashiru Yusuph, miaka 26, sukuma, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 1.
3. Abdallah Juma, miaka 28, mshirazi, mwanachuo State University. Amelazwa word namba 1.
4. Ally Sharifu, miaka 24, mshirazi, mwanachuo. Amelazwa word namba 1.
5. Mussa Mkanga, miaka 21, mzanzibari, Mwanachuo. Amelazwa word namba 1.
6. Seifu Fakii juma, miaka 27, mshirazi, mwanachuo State University. Amelazwa word 1
7. Ahamed Mohamed Hassani, miaka 23, Mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 11.
8.Richard Mwasonga, miaka 36, mnyiha, Tingo wa bus, Miyuji Dodoma. Amelazwa word namba 1.
9.Juma Nasoro, miaka 23, mshirazi, mwanachuo State University Zanzibar. Amelazwa word namba 1.
10.Hemedi Mohamed, miaka 29, Mzanzibari, mwanachuo State University Zanzibar. Amelazwa word namba 1.

11. Mussa Mtaugana, miaka 24, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar  University
12. Adam Mwale Bonifasi, miaka 24, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University                      Amelazwa word namba 1.
13.  Mohamed Ally Mohamed, miaka 23, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University.
14.  Nassoro Mohamed Saidi, miaka 25 -30, mwanachuo State University Zanzibar. Hali yake si nzuri sana na amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Aidha Kamanda KAGANDA amesema Chanzo cha ajali ni  mteremko mkali wenye kona iliyosababisha dereva kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha ajali ya gari kupinduka upande wa kulia na kulala kiubavu. Mara baada ya ajali hiyo dereva alikimbia kwenda kusikojulikana na juhudi za kusaka dereva huyo zinaendelea. Pia  uchunguzi unaendelea kubaini iwapo gari hilo lilikuwa na tatizo lolote.

Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma linatoa Wito kwa madereva kila mara wawe makini barabarani hasa kipindi hiki cha mvua na kuwa makini hususani kwa barabara zenye milima.

No comments: