Washindi wa tuzo hiyo chuo kikuu cha Iringa wakiwa na tuzo yao kushoto ni mkuu wa chuo Prof Nicholaus Bangu na kulia wa kwanza na mkuu msaidizi wa kitivo cha sheria Bi Jane Massey |
Mkuu wa chuo cha Tumaini ( chuo kikuu cha Iringa ) Prof Nicholaus Bangu akionyesha tuzo ya heshima ya sheria za kivita ambayo chuo chake kimeiwezesha Tanzania kufanya vema |
Washindi wa tuzo hiyo wakiwa na vyeti vyao katika picha ya pamoja na mwalimu Dr Chachage Tanzania yazibagwa nchi sita barani Afrika katika mashindano ya vyuo vikuu ya kuwania tuzo ya heshima ya sheria za vita yaliyomalizika hivi karibuni . Katika shindano hilo lililofanyika kati ya Novemba 16-23 mwaka huu jijini Arusha chuo kikuu cha Iringa kiliwakilishwa na washiriki watatu ambao ni Anneny Nahum ,Janeth Nagai na Joanna Mcintype vijana hao waliweza kufanya vema kiasi cha kuiwezesha nchi ya Tanzania kuibuka mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo. Wakizungumza leo chuoni hapo katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo hiyo kwa uongozi wa chuo hicho ,washirikia hao walisema kuwa ushindi huo umetokana na ushirikiano ulioonyeshwa na nidham iliyotukuka miongoni mwao. Hata hivyo walisema kuwa tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Tanzania na ni heshima kwa chuo hicho . mkuu msaidizi wa kitivo cha sheria chuo kikuu cha Iringa Jane Massey alisema kuwa washiriki hao wamepata kushinda kutokana na kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika mashindano hayo na kuwa heshima kubwa ambayo chuo hicho imepata ni jambo na kujivunia na kumshukuru Mungu pia. ZAIDI SOMA HAPA |
No comments:
Post a Comment