Social Icons

Monday 8 October 2012

SHEREHE ZA MAHAFALI YA 34 YA BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU


Mhitimu wa Shahada ya CPA ya  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu  ( NBAA)  , Gloria Joel Bendera , akipongezwa kwa kuoena mikono na Mgeni rasmi  Naibu Waziri wa Fedha , Janet Mbene  , baada ya kkumtunuku Shahada yake wakati wa Sherehe ya Mahafali ya 34 ya Bodi  hiyo yaliyofanyika Oktoba 6, 2012 kwenye viwanja vya Mhasibu , Barabara ya Biti Titi Momamed, Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahitimu wa  mahafali ya 34 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu  ( NBAA)  wakifurahia jambo wakati wa mazungunzo yao baada ya kutunikiwa Shahada ya CPA,  Oktoba 6, mwaka huu na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha , Janet Mbene ( hayupo pichani)  katika  viwanja vya Mhasibu , Barabara ya Biti Titi Momamed, Dar es Salaam , Naibu Waziri huyo pia aliwatunukia wahitimu wengie vyeti .
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kati kati ) na Mkewe mama Bendera akiwa katika  picha na mtoto wao,  Gloria Bendera , baada ya kutunikiwa Shahada ya CPA , Oktoba 6, 2012 wakati wa  mahafali ya 34 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu  ( NBAA) ,Mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Fedha , Janet Mbene ( hayupo pichani) kwenye  viwanja vya Mhasibu , Barabara ya Biti Titi Momamed, Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( wapili kutoka kulia) akiwa  katika  picha na  baadhi ya wahitimu wa  mahafali ya 34 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu  ( NBAA) wakiwa mtoto wake , Gloria Bendera ( watatu kulia mwenye mkoba mkononi)  baada ya kutunukiwa Shahada na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha , Janet Mbene ( hayupo pichani)  Oktoba 6, 2012 katika  viwanja vya Mhasibu , Barabara ya Biti Titi Momamed, Dar es Salaam.
wadau wakifurahia Nondozzz zao. Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro

No comments: