Mgombea nafasi ya Makamu wa Urais wa Seikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Tumaini-Iringa (TUSO-IUCO) Judith Kahwa akimwaga sera zake.
Mgombea nafasi ya Urais wa Seikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Tumaini-Iringa (TUSO-IUCO) Mchungaji Joshua Chusi akimwaga sera zake.
Mgombea nafasi ya Urais wa Seikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Tumaini-Iringa (TUSO-IUCO) Mauna Chuma Belius akimwaga sera zake.
KAMPENI za Uchaguzi Mkuu wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Tumaini-Iringa (IUCO) zinazidi kupamba moto huku wagombea mbalimbali wakipita kunadi sera zao katika madarasa, Hostel na maeneo mbalimbali chuoni hapa.
Viongozi hao wanaowania nafasi mbalimbali za kuiongoza Serikali ya Wanafunzi chuoni TUSO-IUCO wanafanya kampeni hizo tayari kwa uchaguzi baada ya kipindi cha uongozi wa Serikali iliyipo madarakani kumaliza muda wake.
Serikali iliyopo madarakani chini ya Rais wake Method Kagoma inafikia ukomo wake kesho Aprili 21, 2012 baada ya kufanyika uchaguzi mkuu.
Taarifa kutoka Tume ya Uchaguzi Chuoni hapo inasema watakaokuwa na sifa ya kupiga kura hiyo kesh ni wanafunzi wote halali wa Chuo hicho cha Tumaini Iringa.
Aidha Tume hiyo inasema kuwa Mwanafunzi halali ni Yule aliye na kitambulisho, hivyo asiye na kitambulisho atakosa haki yake ya msingi ya kupiga kura kuchagua viongozi wake katika uchaguzi huo.
Nafasi zinazowaniwa katika Uchaguzi huo ni pamoja na nafasi ya Rais, Makamu wa Rais, pamoja na wawakilishi wa Vitivo (wabunge) na wawakilishi wa Maeneo (Madiwani) ambao wote watapigiwa kura hiyo kesho.
Wagombea mbalimbali wamekuwa wakipita hapa na pale ikiwa ni pamoja na kubandika picha zao katika kuta ikiwa ni sehemu ya kutafuta kura.
Habari kwa hisani ya Blog ya Father Kidevu
No comments:
Post a Comment