Social Icons

Wednesday 11 January 2012

CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII (CDTI) CHAMWAGA MISAADA KWA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA NA WAISHIO MAZINGIRA HATARISHI.

Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI) mkoani Mbeya jana kimetembelea katika kituo cha Nuru Orphans na kutoa misaada ikiwemo Unga, mchele, sabuni, mafuta ya kula, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 463,000 zilizochangwa na wanachuo hao kuunga mkono, juhudi zinazofanywa na kituo hicho kinacholea watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi. Kituo hicho kina jumla ya watoto 14 kilichopo maeneo ya Uyole Kati jijini Mbeya.
Wanachuo wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI) mkoani hapa wakiwa nje ya chuo chao jana, wakijiandaa kuelekea katika kituo cha Nuru Orphans na kutoa misaada ikiwemo Unga, mchele, sabuni, mafuta ya kula, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 463,000 zilizochangwa na wanachuo hao kuunga mkono, juhudi zinazofanywa na kituo hicho kinacholea watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi. Kituo hicho kina jumla ya watoto 14 kilichopo maeneo ya Uyole Kati jijini Mbeya.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI) na Mkufunzi Bwana John Mogha akitoa taarifa ya chuo hicho jinsi kinavyothamini na kujali vituo vya kulelea watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi ikiwa ni moja ya kazi za wanavyuo hao, ambapo ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali kusaidia vituo hivyo. Hata hivyo jana wanachuo wa chuo chake walitembelea katika kituo cha Nuru Orphans na kutoa misaada ikiwemo Unga, mchele, sabuni, mafuta ya kula, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 463,000 zilizochangwa na wanachuo hao kuunga mkono, juhudi zinazofanywa na kituo hicho kinacholea watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi. Kituo hicho kina jumla ya watoto 14 kilichopo maeneo ya Uyole Kati jijini Mbeya.
Mlezi wa kituo cha Nuru Orphans Bi Amanda Fyabango akionesha malazi wanaolazwa watoto wanaookotwa mitaa na kuwalea kama familia moja, na kwamba kituo hicho kimeanza mwaka 2008 kikiwa na watoto wawili ambapo kwa sasa kinanjumla ya watoto 14. Aidha ameeleza chanzo kikuu cha watoto kutupwa ni kutokana na wananume kukataa mimba, kutelekeza wake zao na ugumu wa maisha. Ameongeza kuwa wanawake na mabinti wanapopata mimba wasiitoe.
Baadhi ya wanachuo wakiwa wamebeba sehemu ya msaada huo uliotolewa katika kituo cha Nuru Orphans.
Sehemu ya misaada iliyotolewa ikiwemo sabuni, mafuta, sukari na unga.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini waliunga mkono juhudi hizo za wanachuo hao na kutoa wito kwa jamii mbalimbali kutoa misaada kwa vituo vya kulelea watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi kwani ni jukumu letu sote. Kutoka kushoto ni Cheyo(TBC1), Karanja Njuguna(ITV) wakiwa na waratibu wa utoaji wa misaada hiyo.
Baadhi ya watoto wakiwa katika picha ya pamoja na wanachuo cha Maendeleo ya Jamii.
Mmoja kati ya wanachuo wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii akisoma risala baada ya jana kutembelea katika kituo cha Nuru Orphans na kutoa misaada ikiwemo Unga, mchele, sabuni, mafuta ya kula, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 463,000 zilizochangwa na wanachuo hao kuunga mkono, juhudi zinazofanywa na kituo hicho kinacholea watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi. Kituo hicho kina jumla ya watoto 14 kilichopo maeneo ya Uyole Kati jijini Mbeya. Hata hivyo wameitaka Jamii kusaidi watoto kwani sehemu ya maendeleo. (Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya).

No comments: