Social Icons

Thursday 1 December 2011

Leo ni siku ya UKIMWI Duniani ... Walaka maalum kwa wanavyuo vikuu wote Tanzania

Ndugu wasaomi taifa la Kesho, na Kizazi kijacho ambacho mnategemewa kuleta maendeleo makubwa Mbeleni Je umewahi kujiuliza ya Kuwa wewe ni moja ya Dhahabu hapa Nchini?... Kama majibu ni ndio basi leo ni siku maalum kabisa ya UKIMWI Duniani Je umeima afya yako na kujikuta upo salama? Je kama Umeathirika kwa nini unaeneza maambukizi kwa wenzako?? katika siku kama ya leo ni ya kujiuliza sana kama wewe kijana mdogo unaetegemewa na mwenye elimu yako nzuri sana kwa nini ufe mapema? ndugu jamaa marafiki na taifa kwa ujumla linakuangalia pia hivyo basi ndugu zangu wanafunzi tuwe macho sana, Najua kuna dada zetu ambao wao wanazidi danganyika kwa vitu vidogo na kuishia mtegoni na pia kupata maambukizi haya ya Gonjwa hatari, Hivyo Basi tunawaomba kuwa makini sana, Hata kaka zetu ambao mnatumia nafasi ya uanachuo kikuu na kuwarubuni watoto wa sekondari kwa Ngono uzembe yani ya kuto tumia Kinga ya Condom pia tuwe makini sana huwezi mwangalia na kumtambua huyu ana ukimwi ama la maana hawana Nembo, Chukua Tahadhari sasa.. wewe nawenzako pia, Tumewaandikia walaka huu. Mwisho kabisa Tusiwanyanyapae walio Athirika na maambukizi haya ya UKIMWI 
Asanteni sana,
Imeletwa kwenu na wenzenu
Matukio na wanavyuo Crew

No comments: