Social Icons

Thursday, 3 November 2011

USIKU WA BAGAMOYO INTERCOLLEGES NIGHT 2011 ulivyoinogesha BAGAMOYO


KIM KIMENYA MKURUGENZI WA KIMKEV ENTERTAINMENT AKIKABIDHI ZAWADI YA FEDHA TASLIM KWA MSINDI WA SWALI LA USIKU WA BAGAMOYO INTERCOLLEGES NIGHT 2011 DADA MANKA KUTOKA SLADS..
KIM KIMENYA MKURUGENZI WA KIMKEV ENTERTAINMEN AKISOMA
SALAMU ZA UFUNGUZI WA BAGAMOYO INTERCOLLEGES NIGHT 2011.
GESASE MRIMI AKITANGAZA ZAWADI ZA LADY OF THE NIGHT NA MAN OF NIGHT.KUSHOTO AISHA KIPUTULA LADY OF NIGHT,KATI FRANCIS KAMULI MAN OF THE NIGHT.
MSANII DULAYO D-TIMING AKIWAPAGAWISHA MASHABIKI,
MASHABIKI WAKIPAGAWISHWA NA DULAYO D-TIMING

==== ======== ====== ========




USIKU WA BAGAMOYO INTERCOLLEGES NIGHT 2011
WAIBAMBA BAGAMOYO

Usiku wa Bagamoyo intercolleges Night uliyofanyika usiku wa tarehe 28.10.2011(Ijumaa) umeanza kwa aina kasi yake baada ya kuweza kuzikonga nyoyo za wanachuo na wasio wanachuo waliojitokeza kwa wingi kushuhudia huo wa kitaaluma na burudani ulifanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya vyuo vya mji wa Bagamoyo.

Usiku huo ambao ulivishirikisha vyuo vya Bagamoyo kikiwemo Tasuba,Adem,Mbegani,SLADS,na BIT umeacha gumzo katika viunga vya mji huo kwa namna ulivyoendeshwa kwa umakini mkubwa na kumaliza kiu ya mashabiki wa burudani.

Kwa upande wa burudani, tukio hilo la kihistoria lilipambwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiongozwa na Dulayo D-Timing aliyewapagawisha washabiki waliofurika katika ukumbi wa TaSUBa na wimbo wake wa “twende zetu mchumba”.Mwisho wa buradani ulikwa muziki wa disko ulichanganywa kwa ustadi mkubwa na dj Nature Skills.

Sambamba na burudani ya muziki wa kizazi kipya na disko, ndani ya usiku huo pia alipatikana mshindi wa swali la usiku huo ambaye alijipatia fedha taslimu.Pia alipatikana “Lady of the night” ambaye alikuwa Aisha Kiputula na “Man of the night” alikuwa Francis Kamuli ambao kwa pamoja walizawadiwa zawadi ya fedha taslimu na nafasi ya kupumzika katika hoteli ya Green Park Village iliyopo Mjini Bagamoyo.Lady of the night na man of night walipatikana baada ya kupendeza kwa kuvaa nyeupe,

Akizungumza mchana wa leo Bw. Kim Kimenya Mkurugenzi wa Kampuni ya Kimkev Entertainment alisema anawashukuru sana wanachuo na wasio wanachuo kwa kujitokeza kwa wingi na kuahidi kuliboresha zaidi tukio hilo kwa mwaka ujao kwa kuongeza michezo ya aina mbalimbali.

Kimenya aliongeza kuwa kwa kuwa Chuo cha ukutubi na utunzaji wa nyaraka (SLADS) ndicho kilichotia fora kwa kujitokeza kwa wingi kuliko vyuo vingine.”Tupo kwenye maandalizi ya kuwafanyia wanachuo wa chuo hiki kwa kuwa walijitokeza kwa wingi na kushinda zawadi zote”alsema Kimenya. sherehe fupi ya kuwapongeza SLADS inatarajia kufanyika hivi karibuni.

Usiku wa Bagamoyo intercolleges Night ni tukio endelevu lenye lengo la kuwaunganisha na kuwaburudisha wanavyuo wa mji wa Bagamoyo na miji ya jirani ambao umepangwa kufanyika kwa kila mwaka. www.Kimkeventertainment.blogspot.com

No comments: