Social Icons

Saturday 5 November 2011

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI AWAPA TAHADHALI WAKAGUZI WA KANDA MKOANI ARUSHA

a
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mh. Philipo Augustino Mulugo akikabithi kiti cha mwalimu ambaye ni mlemavu (hayupo pichani) ambacho atakitumia kutembelea pindi aendapo shuleni kufundisha.
Walimu wa Wilaya ya Arumeru wakicheza katika sherehe za maadhimisho ya siku ya mwalimu duniani na miaka 50 ya chama cha walimu Tanzania,anayeimba katikati ni Mwalimu Saimoni ambaye alikuwa anaburudisha walimu wenzake mbele ya mgeni rasmi.

Na Woinde Shizza,Arusha

SERIKALl imesema kuanzia mwakani itakuwa katika mchakato wa kuanda waraka ambao utasambazwa kwa wakaguzi wa kanda,waratibu wa elimu watakutana na wakuu wa shule za msingi kote nchini,ambapo wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza watatakiwa kuwa ni wale waliofaulu tu.

Naibu Waziri wa Elimu Mafunzo na ufundi Philip Mulugo aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya walimu duniani,yaliyofanyika Wilayani Arumeru,mkoani hapa..

Naibu huyo alisema kuwa atawawajibisha wakuu wote wa shule za msingi ambao watabainika kuwafaulisha wanafunzi na kuingia kidato cha kwanza bila kujua kusoma wala kuandika.

Akizungumzia suala la shule ambazo hazijasajiliwa aliwataka waratibu wa elimu wa kata kuwajibika kwa madai kuwa shule nyingi zimekua zikiendeshwa bila kusajiliwa kutokana na waratibu watendaji wa elimu kutowajibika kuanzia ngazi za chini.

Aliendelea kusema kua serikali imepanga kutoa posho ya shilingi laki tano kwa waajiriwa wapya wanaporipoti katika vituo vipya na vitakavyoainishwa kuwa viko katika mazingira magumu.

Naye Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Arusha Nuru Shemkaro aliwataka walimu hao kuwa na mshikamano na chama chao ili kuweza kutimiza majukumu na kutetea haki zao.

Aidha aliiomba serikali kutatua changamoto zinazowakabili walimu ikiwa ni pamoja kuongezewa kwa mishahara pale wanapopandishwa madaraja ili waweze kujikimu kimaisha kwani walimu wengi wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu kutokana na mishahara yao kua midogo.

No comments: