Social Icons

Thursday 22 September 2011

Serikali ya Uholanzi imeipatia serikali ya Tanzania Euro Milioni 15 ambazo ni zaidi ya Bilioni 30 kuboresha elimu ya juu nchini.



Tanzania itafaidika na msaada wa Euro Milioni 15 (Zaidi ya Bilioni 30) toka serikali ya Uholanzi kugharimia mradi wa Kujenga Uwezo kwa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini, unaojulikana kwa jina la NICHE (Netherlands Initiative for Capacity Development in Higher Education).
Hayo yamebainishwa na Meneja wa mradi huo, Bi. , alipotembelea Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro, kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ambao kwa chuo kikuu hicho, mradi huo unatoa ufadhili kwa Shule ya Biashara na kuboresha mafunzo ya utawala wa Serikali za Mitaa.
Bibi Jansen, amesema ana matumaini makubwa sana kuwa mradi huu utakapokamilika, utaboresha sana zile sekta zilizoainishwa kwenye mradi huu ambazo ni kujenga uwezo katika kutoa elimu kuhusu Afya, Sekta Binafsi na Serikali za Mitaa.
Kwa upande wake, msimamizi wa mradi huo hapa nchini Tanzania, kupitia Shirika la NUFFIC, Bibi Johanna Van Nieuwenhuizen, amesema Uholanzi imeridishwa sana na jinsi Tanzania inavyoitumia misaada toka nchini mwake, hivyo kujihakikishia fursa zaidi za kusaidiwa katika miradi mbalimbali.
Naye Naibu Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof. Mugishi Nkwabi Mgasa, aliemwakilisha Makamo Mkuu wa Chuo, aliishukuru serikali ya Uholanzi kwa kufadhili mradi huo na kueleza kuwa ufadhili huo unamaana kubwa sana kwa Chuo Kikuu cha Mzumbe, kwa sababu utapanua uwezo wa chuo hicho katika kutoa mafunzo ya biashara na utawala wa serikali za mitaa.
Naye mkuu wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dr. Joseph Kimeme, amesema ufadhili huo, utawafanya wanafunzi wanaomaliza Shele ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, sio tuu kuhitimu kwa elimu yenye ubora wa hali ya juu, bali pia watajengewa uwezo wa kujiajiri kwenye kuanzisha biashara zao wenyewe kufuatia mahitaji ya soko.
NICHE ni mradi unaofadhiliwa na serikali ya Uholanzi kupitia Shirika lake la Kimataifa Ushirikiano kuboresha Elimu ya Juu, NUFFIC. Kwa hapa nchini, mradi huo, unaafadhili miradi mbalimbali ya kujenga uwezo katika sekta za Afya, Maboresho ya Sekta Binafsi na Ugwatuaji wa madaraka kwa Serikali za Mitaa.
Kwenye sekta ya Afya, mradi utajikita kwenye kujenga uwezo utoaji elimu ya afya ili kuboresha wahitimu watakao ajiriwa katika utuaji wa huduma kwa mama na motto ili kupunguza vifo vya uzazi na watoto wa umri wa chini ya miaka mitano.
Kwa upande wa elimu ya biashara, mradi utafadhili utoaji wa mafunzo ya elimu ya biashara kwa kuwajengeo uwezo wa wahitimu, kujiajiri moja kwa moja kwa kuanzisha biashara zao, hivyo kuyondokana na wahitimu wa elimu ya biashara wanaosubiri kuajiriwa.
Kwa upande wa Serikali za Mitaa, mradi huu utajikita katika kuwajengea uwezo maofisa za serikali za mitaa katika suala zima la ugwatuaji wa madaraka ya kubuni miradi na kusimamia utekelezaji wao wenyewe badala ya kuitegemea serikali kuu. Kwa sasa serikali nyingi za mitaa zinasubiri kupelekewa miradi ya maendeleo toka serikali kuu ambayo ndio huigharimia, lakini maendeleo ya kweli yanaletwa na wananchi mmja mmoja au katika vikundi kutokea chini kwenye serikali za mitaa.

No comments: