Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ulioanza leo tarehe 6 na unatarajiwa kumalizika tarehe 8 november, katika ukumbi wa APC Bunju, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipata maelezo ya namna ya mashine ya kuchora kadi za mifumo ya umeme
inavyofanya kazi na Mhandisi Vedastus Sichilima kutoka D.I.T (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan, leo amefungua Mkutano wa Kimataifa wa wadau wa elimu na mafunzo
ya ufundi. Mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya
APC Bunju wilayani Kinondoni, umeandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu
ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikianana Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ya
nchini Finland.
Akihutubia
washiriki katika Mkutano huo wenye kaulimbiu isemayo “wekeza katika
elimu ya ufundi na mafunzo kwa Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda”
Makamu wa Rais alisema kaulimbiu hiyo inaenda sambamba na agenda ya
serikali ya kutekeleza dira ya kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati
ifikapo 2025. “Ni dhahiri kuwa elimu ya ufundi ni nguzo muhimu ya
kufikia agenda ya serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda na kufikia uchumi
wa kati ifikapo 2025” alisisitiza Makamu wa Rais
Makamu
wa Rais alisema amefarijika kuona kuwa Mkutano huo umepambwa na magwiji
wote kutoka taasisi na vyuo vya elimu ya ufundi pamoja na wadau wote wa
utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo. Aidha, alisisitiza kuwa anatambua
kuwa kutoa elimu ya ufundi ni mkakati muhimu sana utakaosaidia kubadili
fikra na mitazamo ya raia walioelimika na kuwa mahiri katika stadi na
maarifa ya kutosha kusaidia kukabiliana na changamoto za maendeleo ya
nchi yetu.
Sambamba
na hilo, Makamu wa Rais aliwapongeza waajiri waliojitokeza katika
mkutano huo na kuwaasa kwamba wao ni kiungo muhimu sana katika kuleta
maana halisi ya mkutano huo. Makamu wa Rais alisema ili kuzalisha na
kuendeleza rasilimali watu bora katika kada ya kati ni lazima kuwepo
mahusiano mazuri baina ya taasisi zinazotoa mafunzo ya ufundi na
waajiri. Mahusiano hayo ndiyo yatakayozalisha wataalam bora kwa ajili ya
maendeleo ya Taifa letu.
Akizitaja
changamoto zinazoikabili sekta ya elimu hapa nchini, Makamu wa Rais
alisema ni pamoja na kutokuwepo kwa muunganiko wa kutosha kati ya
taasisi zinazotoa elimu na mafunzo ya ufundi na waajiri kama vile
viwanda, mabenki, taasisi za afya na vyombo vya habari. Aidha, upo
uelewa mdogo miongoni mwa wadau na jamii kwamba elimu ya ufundi inahusu
masuala ya useremala, uashi, ufundi makenika, kushona nguo na mambo
yanayofanana na hayo. Pamoja na hayo upungufu wa miundombinu stahiki
katika vyuo vya ufundi ili kutoa mafunzo yenye viwango vya ubora wa hali
ya juu nayo ni changamoto.
Makamu
wa Rais alisema wakati nchi inaelekea kwenye uchumi wa Viwanda, hatuna
budi kujipana kuandaa wataalamu wa kutosha hivyo Serikali imeelekeza
Baraza kuanda, kupitia upya na kuboresha Mitaala kwenye maeneo muhimu
ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.
Makamu
wa Rais alisisitiza kuwa utoaji wa Elimu ya Ufundi inayojibu matatizo
ya jamii, inayoandaa vijana wenye umahiri wa kuweza kupambana na
changamoto za maendeleo katika ulimwengu wa sasa wa Sayansi na
Teknolojia.
Mwisho
Makamu wa Rais alisema kuwa ni matarajio yake Mkutano huu utatoa
maazimio na ufumbuzi wa namna ya kukabiliana na changamoto za utoaji wa
Elimu ya ufundi na kuishauri Serikali ipasavyo juu ya hatua za kuchukua
ili elimu itolewayo iendane na mahitaji ya Soko la ajira.
Makamu
wa Rais aliwashukuru na kuwapongeza Taasisi ya Elimu ya watu Wazima ya
Finland kwa kushirikiana na NACTE katika kuandaa mkutano huo .
Aidha aliwapongeza Jamhuri ya Watu wa Finland kwa kuadhimisha miaka 100 ya uhuru.
No comments:
Post a Comment