Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa sheria namba 8 ya mwaka 2011.
Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege inatangaza nafasi za Kazi katika maeneo
yaliyoainishwa hapo chini, kwa wazanzibar wenye sifa zinazohitajika.
1. OFISA USALAMA DARAJA LA I I (AVIATION SECURITY OFFICER GRADE II) Nafasi 10 Unguja
Sifa ya kuingia kazini
Mwenye
Shahada ya Kwanza/Stashahada ya Juu au Stashahada ya Uzamili katika
fani ya Mifumo ya Kompyuta (IT) au Sheria au Sayansi ya Jamii au Utawala
au Menejimemti ya Rasilimaliwatu kutoka chuo kinachotambuliwa na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
1. OFISA USALAMA MSAIDIZI DARAJA LA III (AVIATION SECURITY ASSISTANT OFFICER GRADE III) Nafasi 40 Unguja
Sifa za Kuingilia Kazini
Mwenye
Stashahada ya Mifumo ya Kompyuta (IT) au Sheria au Sayansi ya Jamii au
Utawala au Menejimemti ya Rasilimaliwatu kutoka chuo kinachotambuliwa
na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
2. MHANDISI MITAMBO (MECHANICAL ENGINEER) Nafasi 1 Unguja
Sifa za Kuingilia Kazini
Kuajiriwa
mwenye Shahada ya Kwanza/Stashahada ya Juu au Stashahada ya Uzamili
katika fani ya Mitambo au fani nyengine inayolingana nayo kutoka katika
chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
3.MHANDISI MAJENGO (CIVIL ENGINEER) Nafasi 1 Unguja
Sifa za Kuingilia Kazini
Kuajiriwa
mwenye Shahada ya Kwanza/Stashahada ya Juu au Stashahada ya Uzamili
katika fani ya Ujenzi au fani nyengine inayolingana nayo kutoka katika
chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
2. MHANDISI UMEME (ELECTRICAL ENGINEER) Nafasi 1 Unguja
Sifa za Kuingilia Kazini
Kuajiriwa
mwenye Shahada ya Kwanza/Stashahada ya Juu au Stashahada ya Uzamili
katika fani ya Umeme au fani nyengine inayolingana nayo kutoka katika
chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
3. OFISA MAZINGIRA (ENVIRONMENTAL OFFICER) Nafasi 1 Unguja
Sifa za Kuingilia Kazini
Mwenye
Shahada ya Kwanza/Stashahada ya Juu au Stashahada ya Uzamili katika
fani ya Sayansi/Sanaa ya Mazingira au fani nyengine inayolingana nayo
kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ).
4. FUNDI MCHUNDO UMEME DARAJA LA III ( Nafasi 1Unguja na 1 Pemba )
Sifa za Kuingilia Kazini
Mwenye
Stashahada ya kawaida au FTC katika fani ya umeme au cheti chengine
kinachofanana na hicho kutoka katika taasisi inayotambulika na serikali.
5. FUNDI SANIFU UMEME DARAJA LA III ( Nafasi 3 Unguja )
Sifa za Kuingilia Kazini
Mwenye
cheti katika fani ya Umeme au fani nyengine inayolingana nayo kutoka
katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ).
6. FUNDI SANIFU KUCHONGA (CARPENTER) Nafasi 1 Unguja
Sifa za Kuingilia Kazini
Mwenye
cheti katika fani ya ufundi kuchonga au fani nyengine inayolingana
nayo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar (SMZ).
7. FUNDI SANIFU KUCHONGA (ALLUMINIUM) Nafasi 1 Unguja
Sifa za Kuingilia Kazini
Mwenye
cheti katika fani ya ufundi kuchonga au fani nyengine inayolingana
nayo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar (SMZ).
8. FUNDI MCHUNDO BOMBA (PLUMBER) DARAJA LA III ( NAFASI 1 UNGUJA)
Sifa za Kuingilia Kazini
Mwenye
Stashahada ya kawaida au FTC katika fani ya Ufundi Bomba au cheti
chengine kinachofanana na hicho kutoka katika taasisi inayotambulika na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
9. MUEGESHA NDEGE MSAIDIZI DARAJA LA III (nafasi 6 Unguja, 2 Pemba)
Sifa za kuingilia kazini
Mwenye
cheti cha kidatu cha nne pamoja na cheti cha masomo ya Uegeshaji wa
Ndege (Appron Management) au cheti kinachofanana na hicho ambacho
kimetolewa na Mamlaka inayotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar (SMZ).
10. KATIBU MUKHTASI DARAJA LA III ( Nafasi 3 Unguja)
Sifa za kuingilia kazini
Mwenye Diploma/Stashahada ya fani ya Uhazili kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
11. OFISA BIASHARA DARAJA LA II ( nafasi 1 Unguja na 1 Pemba)
Sifa za Kuingilia Kazini
Mwenye
Shahada ya Kwanza/Stashahada ya Juu au Stashahada ya Uzamili katika
fani ya Masoko, Biashara, Utawala na Uchumi, Sheria za Kibiashara au
fani nyengine inayolingana nazo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
12. MHASIBU MSAIDIZI DARAJA LA III (nafasi 1 Pemba)
Sifa za kuingilia kazini
Mwenye Stashahada ya kawaida ya Uhasibu au Uongozi wa Fedha kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
13. MHUDUMU VIP DARAJA LA II (nafasi 2 Pemba)
Sifa za kuingilia kazini
Mwenye
cheti cha kidatu cha nne au sita na hicho kutoka katika mamlaka
inayotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Mwenye uzoefu
wa kuwahudumikia viongozi atapewa kipau mbele.
14. DEREVA DARAJA LA III (nafasi 1 Pemba)
Sifa za kuingilia kazini
Mwenye
cheti cha Kidato cha nne aliyefaulu na kupata leseni ya gari kutoka
katika Mamlaka inayotoa leseni na kutambuliwa na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar.
15. a) OFISA WA MIFUMO YA KOMPYUTA DARAJA LA II (System Administrator) nafasi moja Unguja na moja Pemba
b) OFISA WA MITANDAO YA KOMPYUTA DARAJA LA II (Net Works Engineer) nafasi moja Unguja.
c) OFISA WA KUKIMU MIFUMO YA KOMPUTA (IT Service/Support Engineer) nafasi moja Unguja
d) OFISA MUENDELEZAJI MIFUMO YA KOMPUTA (System Developer) nafasi mbili Unguja
Sifa za kuingilia kazini
Mwenye
Shahada ya Kwanza /Stashahada ya Juu au Stashahada ya Uzamili katika
fani ya Sayansi ya Kompyuta/habari ya Kompyuta au fani nyengine
inayolingana nazo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
• Kufanya kazi nyengine zinazolingana na kazi yake kama atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
Jinsi ya Kuomba
Barua za maombi zielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
S.L.P 4742
Zanzibar
Barua
hizo ziambatanishwe na taarifa binafsi ya muombaji (CV), Vivuli vya
Cheti cha kuzaliwa, Kitambulisho cha Ukaazi cha Zanzibar na vyeti vya
masomo.
Siku ya mwisho ya kupokea maombi hayo ni siku ya Jumatano ya tarehe 04/08/2017.
No comments:
Post a Comment