CHUO Cha Usimamizi wa Fedha nchini (IFM) kimetenga mda wa wiki moja
kwa ajili ya kutoa ufafanuzi, maelekezo na kufanya udahili wa kozi
mbamlimbali zinazotolewa na chuo hicho.
Mkuu wa Kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii katika Chuo Hicho Bwana
Kadida Mashaushi alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa zoezi hilo
litaanza tarehe 29 mwezi huu na kumalizika tarehe 5 mwezi ujao (8)
katika Chuo hicho kilichopo jijini hapa.
“Kwa wale wakazi wa Dar es Salaam na wale wa mikoa ya jirani, fursa
hii ambayo imetolewa na chuo cha usimamizi wa fedha nchini ni adimu kwa
kutoa maelekezo kwa wazazi, wanafunzi watarajiwa, waombaji na wadau
mbalimbali kuzielewa kwa usahihi kozi mbalimbali ambazo zinatolewa na
chuo,” alisema.
Bwana Mashaushi alisema kuwa zoezi hilo ni mwitikio wa chuo hicho
baada ya serikali kutoa muongozo kwa namna ambavyo wanafunzi wapya wa
elimu ya juu watadahiliwa mwaka huu wa masomo (2017/18) na maelekezo
yaliotolewa kuhusu vigezo vya kuingia elimu ya juu.
Alisema kutokana na maelekezo hayo, kumekuwepo na mkanganyiko
miongoni mwa wa wadau mbalimbali kwenye sekta ya elimu ya juu hususani
kwa upande wa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini,
hivyo kupelekea chuo hicho kuanzisha hilo zoezi kwa ajili ya kusaidia
katika kutatua changamoto hizo.
“Zoezi hili litasaidia wale ambao wanatamani kuingia elimu ya juu,
kuwawekea wepesi wa kutosha ili kufanikisha malengo yao,” alisema na
kuongeza kuwa katika zoezi hilo, chuo hicho kinatoa maelekezo ya kina na
kujibu maswali yale ambayo jamii kwa ujumla imekanganyikiwa baada ya
mabadiliko ya udahili yalitolewa mwaka huu na serikali.
Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni uelewa usietosheleza kwa
muomba na kupelekea baadhi ya wao kuomba kozi ambayo hana sifa nayo na
ombi lake kwenda kwa katika kozi mabayo sio sahihi na baadaye
kutochaguliwa.
Bwana Mashaushi alisema pia wakati huohuo vyuo navyo huenda viakapata
wanafunzi wachache katika zile nafasi ambazo zipo. Zoezi la udahili kwa
wanafunzi wa elimu ya juu linatrajiwa kusitishwa tarehe 30 mwezi ujao
(8) mwaka huu.
“Changamoto kubwa kwa vyuo kutokua ufafanuzi ili kila mwenye alama
zinazotosheleza akapata kuomba kwa usahihi kwa mujibu wa vigezo
viliwekwa na serikali, vyuo na taratibu ambayo serikali imeweka mwak
huu,” aliongeza.
Kwa hatua nyingine, Bwana Mashaushi alisema kuwa kwa wale wa mikoa ya
mbali, watapata taarifa mbalimbali kuhusu udahili wa mwaka huu kupitia
tovuti ya chuo ambapo pia watapata fomu ya maombi ya kujiunga na chuo.
“Kwa wale wa Mwanza watapata maelekezo, ufafanuzi katika kituo chetu
cha mafunzo kilicho huko ambapo watakutana na maaofisa wetu. Na wale
wengine ambao pia hawataweza kufika wanaweza kutumia tovuti yetu na njia
ya posta katika kuwasilisha fomu zao,” alisema.
IFM imejikita katika kutoa kozi za uhasibu ngazi ya shahada,
stashahada na cheti. Pia chuo hicho kimejikita katika fani ya bima na
hifadhi ya jamii ambapo halikadhalika inatolewa kozi ya shahada kozi ya
bima na hifadhi ya jamii na kozi maeneo ya kodi kwenye ngazi ya shahada,
stashahada na cheti.
“Chuo pia kiko vizuri na miongoni mwa vyuo vichache ambavyo vinatoa
mafunzo katika maswala ya bank na fedha katika ngazi ya shahada
(Bachelor of banking and finance) na stashahada (ordinary diploma in
banking and finance) na cheti kwa wanafunzi watarajiwa elimu ya juu.
CHANZO HABARI LEO
No comments:
Post a Comment