Afisa Matekelezo kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Albert Feruzi akitoa elimu kuhusu Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa wanafunzi wa Chuo cha St. John Dodoma hivi karibuni.
Meneja wa Mpango wa uchangiaji wa hiari Bi. Mwajaa Sembe akiwaelezea wanafunzi umuhimu wa kujiwekea akiba kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS)
Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mrisho Mpoto akiwahamisasha wanafunzi wa Chuo cha St. John kujiunga na Mfuko huo.
Mtoa mada Bw. Husein Chanzi akitoa Dondoo kwa wanachuo wa St. John kuhusiana na mambo muhimu ya kuzingatia pindi wanapokwenda katika usaili 'interview'
Baadhi ya wanachuo wa St. John wakiwa wanaendelea kusikiliaza mambo mbalimbali yanayohusiana na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambapo wanachuo 241 walijiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS)
Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mrisho Mpoto akiwahamisasha wanafunzi wa Chuo cha Mipango kujiunga na Mfuko huo.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Mipango Dodoma wakiwa wanaonesha fomu zao za kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wa uchangiajin wa hiari (PSS) ambapo wanachuo 351 walijiunga na mfuko huo.
Wanachuo cha Mipango Dodoma wakiendelea kujaza Fomu za Kujiunga Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS)
Wanachuo wa Chuo cha Mipango Dodoma wakiwa wanasikiliza mambo mbalimbali Muhimu kuhisiana na Mfuko wa Pensheni wa PSPF
No comments:
Post a Comment