Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
KIBAHA
Baraza
la Wauguzi na Wajunga nchini wametakiwa kutowaonea aibu wale wote
wanaoanzisha vyuo vya afya kama mradi wa kujiingizia fedha bila ya kuwa na
taaluma hiyo kwani kunapelekea kuhatarisha Maisha na afya za watanzania.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati
akiweka jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga
kitaaluma nchini lililopo mjini kibaha Pwani.
“Hatusemi wasianzishe vyuo,bali vyuo
vyote viwe vyenye hadhi ya kutoa wataalam stahili ,visajiliwe na vikaguliwe
mara kwa mara ili vizalishe wauguzi wenye sifa na ujuzi stahili,uuguzi siyo
ujasiliamali,hakikisheni mnavifungia vyuo vyote feki ili tuweze kudhibiti
utitiri huu” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy alisema hivi sasa
kumekuwepo na utitiri wa vyuo vingi vya uuguzi ambavyo havijasajiliwa na
havizalishi wauguzi ambao wanastahili kuajiriwa kwenye sekta ya afya na hivyo
kuhakikisha wanasimamia taaluma hiyo na kuvifungia mara moja vyuo vilivyokosa
sifa.
Waziri Ummy alisema kuwa serikali
inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na wauguzi katika hospitali
zote nchini hivyo maboresho yatafanyika na kuhakikisha upatikanaji wa vitendea kazi kwa wauguzi.
“Asilimia 80 za kazi zote katika
hospitali zetu nchini zinafanywa na wauguzi na wakunga hivyo Serikali imesikia
kilio chenu na tutahakikisha tatizo hili tunalitatua” alisema Ummy.
Hata hivyo Waziri Ummy aliwataka wauguzi kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia
maadili na viapo vyao vya kitaaluma kwa
maendeleo ya Afya nchini.
Kwa upande wa Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini
Bi. Lena Mfalila alisema jengo hilo linajengwa
kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza limegharimu pesa ya kitanzania
shilingi bilioni 2.2.
Aidha Bi. Mfalila alisema kuwa ujenzi wa
kituo hicho ulianza Desemba 2015 kwa awamu ya kwanza na kiinatarajiwa
kukamililika na kuanza matumizi yake Januari2017 .
MWISHO.
No comments:
Post a Comment