Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255629914471. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Na: Mwandishi Wetu.
02/11/2016
Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wamempongeza Rais
Magufuli kwa jitihada zake za kuwajali wanyonge hasa katika mambo yanayohusu
elimu.
Pongezi hizo
zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Shirikisho hilo Zenda Daniel
wakati wa mkutano wao na waandishi wahabari kuhusu mambo sintofahamu ya juu ya
mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.
Zenda alisema kuwa
wao kama Shirikisho wanampongeza na kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli kwa jitihada zake za kuwakwamu wanyonge
“Sisi kama Shirikisho
tunampongeza na kumuunga mkono mweshimiwa Rais Magufuli kwa juhudi zake za kuhakikisha
wanyonge wanajikwamua kwakupata elimu bora”. Alisema Zenda.
Pamoja na pongezi
hizo Shirikisho hilo limeelezea masikitiko yake kwa kile kinachoendelea
kuhusiana na suala ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hadi kufikia hatua ya
kultilia shaka uwepo wa baadhi ya watendaji wa Serikali kufanya hujuma ili
kukwamisha azma ya Serikali kutoka mikopo kwa wate wanaostahili.
Katika duku duku lao
walionyesha miongozo miwili tofauti kuhusiana na vigezo vya wanaostahili kupewa
mikopo, mmoja ukitolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia huku mwingine
ukitolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo
walisema vigezo vilivyiwekwa kwenye miongozo hiyo vinakinzana.
Zenda aliongeza kuwa
hata pale wanaposema kigezo cha watoto uyatima kinapopaswa kutumika kumekuwa na
changamoto kwani kuna baadhi ya wanachuo ambao wamethibitika kuwa ni yatima
lakini hawajapewa mkopo hadi sasa.
Aidha walitumia
nafasi hiyo kutoa ushauri kwa Serikali kupitia Wizara husika kukaa pamoja na
Bodi ya Mikopo ili kupitia upya vigezo vinavyotumika kuwapata wanafunzi
wanaostahili mikopo hiyo.
Kwa upande wake
Katibu wa Hamasa wa Shirikisho hilo Nganwa Nzota alitoa angalizo kwa Bodi ya
Mikopo kwa hatua yake ya uhakiki ambapo imelenga kuwaondoa wale wote watakao
kuwa hawana sifa kulingana na vigezo vya sasa kuwa italeta mkanganyiko mkubwa
utakasababisha watu waichukie Serikali yao.
Alishauri kuwa zoezi
la uhakiki liendelee lakini lisihusishe kuwaondolea mikopo wanufaika hao
watakaobainika kutokidhi vigezo vya sasa kwani wao tayari wana mikataba nao na
badala yake wajikite kuhakikisha wanakuwa makini kwa waombaji wapya.
Katika Mkutano huo
maalum uliohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bwana Hamid S.
Muhina Sherikisho hilo liliiomb Serikali ya Rais Dkt. Jonh Pombe Magufuli
kupitia upya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu hili kuongeza ufanisi wake.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment