Social Icons

Friday, 21 October 2016

Bilioni 3.6 zaokolewa kwa wanafunzi hewa – Rais Dkt. Magufuli

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

 
Na Godfriend Mbuya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema shilingi bilioni 3.6 zimeokolewa kutoka kwa wanafunzi hewa wa shekondari na shule za msingi nchini.

Akizungumza katika uzinduzi wa hosteli za wanafunmzi katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam, Dkta Magufuli amesikitishwa na namna Tanzania kila mahali ukigeuka ni hewa akitolea mfano wa wanafunzi hewa nchini ambao wamegundulika baada ya fedha za elimu bure kuanza kuingia mashuleni.

Tumekuwa tukitoka Shilingi 18.77bilioni kila mwezi kwa ajili ya kutekeleza elimu bure lakini kumekuwa na wanafunzi hewa na shilingi bilioni 3.6 zimeshaokolewa” Amesema Rais Dkt. Magufuli.

Rais ametolea mifano ya wanafunzi hewa katika mikoa ya Mwanza kuna wilaya ina wanafunzi hewa 5,000, Arusha kuna wilaya inawanafunzi hewa 9,000 na Dar es Salaam 7,000.

Aidha Rais amesema hosteli zinazojengwa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kwa sasa zikikamilika zitasaidia kubeba wanafunzi 3840.

Pamoja na hayo Rais amebainisha kwamba zaidi ya trilioni mbili zinadaiwa kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu jambo linalofanya bodi hiyo kukosa fedha za kutosha kujiendesha hivyo amewataka walionufaika kujitokeza kulipa mikopo hiyo na wakikaidi sheria ipo wazi.

Sambamba na hayo Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Elimu pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu nchini kufanya uhakiki upya wa vyuo vikiuu nchini ili kubaini ubora na vigezo.
 

No comments: