Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255629914471. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Watoto
wanafunzi wa Darasa la kwanza kutoka Shule ya msingi ya Zinga wakiwa
wanaweza kusoma vitabu wakiwa na miezi sita tuu ya darasani kupitia
Programu ya Room to read
Watoto
wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi ya Zinga iliyopo Bagamoyo mkoani
Pwani wakiwa wanajifunza matamshi ambapo mpaka sasa wanaelewa vizuri na
hizi ni juhudi kubwa zinazofanywa na Shirika la Room to Read.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Zinga Msafiri Tolla akielezea namna walivyoweza
kunufaika na Programu ya Room to Read ambapo amelishukuru shirika hilo
na ameeleza mafanikio waliyo yapata kutokana na kujengewa Maktaba na
Darasa ikiwa ni pamoja na kuwa imesaidia kupunguza upungufu wa Madarasa,
katika Maktaba imeweza kusaidia kiwango cha usomaji kwa wanafunzi na
kufanya wanafunzi wengi kupenda kusoma shuleni hapo, na imewawezesha
hata wanajamii wanayo izunguka shule kuwa na utaratibu wa kujisomea
katika Maktaba hiyo, mwisho alisema kuwa kwa sasa wanafunzi wanaweza
kujisomea wenyewe bila matatizo
Afisa
Elimu Taaluma Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Bi. Ester Lumato
akielezea umuhimu wa Shirika la Room to Read ambapo katika shule ya
Msingi Zinga walianza kufanya nao kazi kuanzia mwaka 2015,alisema miaka
ya nyuma iliyopita taaruma ilikuwa chini lakini baada ya kuanza kufanya
kazi na Room to Read kiwango hicho cha taaluma kimeongezeka zaidi.
Ameongeza kuwa zamani mwanafunzi alikuwa anamaliza darasa la Saba hajui
kusoma wala kuandika lakini kwa sasa wanamaliza wakiwa wanajua hayo yote
kwa sababu ya shirika hilo kutoa Maktaba na Vitabu vya kutosha, mwisho
alitoa wito kwa Mashirika mengine kujitoa kama Room to Read
Joackim
Kawa Meneja wa mradi wa Usomaji na maktaba kutoka Shirika Room to Read
akielezea miradi ambayo wanaendesha ikiwa katika shule za Msingi
wanatekeleza Mradi wa Maktaba na Kusoma ambapo kuna walimu maalum
katika shule 62 za Bagamoyo wanaandaliwa kuhakikisha wanafunzi wanaweza
kusoma na na kuandika vizuri,ambapo mradi huu umetekelezwa Mkoani
Morogoro pia aliongeza kuwa wanampango wa kupanua wigo zaidi wa miradi
yao katika maeneo mengine nchini Tanzania
Hii
ni maktaba ambayo imewezeshwa na Shirika la Room to Read ambapo kuna
vitabu vya aina mbalimbali vya masomo kuanzia Darasa la Kwanza mpaka la
Saba
Wanafunzi wakiwa wametulia wanasoma vitabu katika maktaba yao ambapo kila mmoja anaamua asome kwa namna gani
Wanafunzi wa Darasa la kwanza wakiwa wanaendelea kusoma
Hapa
kila mmoja anaelewa anacho kisoma hii ni kutokana na kuwa na walimu
ambao wamewezeshwa na Shirika la Room to Read ambapo wamekuwa wanaweza
kusoma na kuandika vizuri
Wanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya ya Msingi Zinga wakiwa wanafurahia kupata Vitabu kutoka Shirika la Room to Read
Wanafunzi wakiwa wanachambua vitabu kwa ajili ya kujisomea katika maktaba ambayo imewezeshwa na Shirika la Room to Read.
Hii ni Maktaba ya Shule ya Msingi ya Kiromo ambayo imewezeshwa na Shirika la Room to Read
Mwalimu
Naomi anangisye ambaye anafundisha darasa la kwanza Shule ya Msingi
Kiromo alieleza kuwa kabla ya Shirika la Room to Read hawajaanza kufanya
kazi katika shule hiyo kulikuwa na shida ya ufundishaji katika madarasa
yao,lakini baada ya Shirika hilo kuanza kazi katika shule hiyo waliwapa
mafunzo ambayo yamewasaidia kwa kiasi kikubwa katika ufundishaji na kwa
sasa wanafunzi wengi wanajiweza katika kusoma, aliwaomba Shirika la
Room to waendelee hivyo ili kuja kutokomeza kabisa tatizo la Ujinga
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kiromo Bi. Flora Mlowe alisema kuwa mradi
wa Room to Read umeinufaisha sana shule yake kwanza wameweza kupata
chumba cha kusomea amacho kimewasaidia sana wanafunzi tofauti na
ilivyokuwa mwanzoni, aliongeza kuwa mradi huo umewafanya wanafunzi
waweze kuongeza juhudi za kujisomea, wanasoma kwa burudani na pia
wanapata maarifa mbalimbali kupitia vitabu hivyo, hiyo imesaidia kuondoa
kundi kubwa la wanafunzi ambao hawajui kusoma alimaliza kwa kusema kuwa
kuwepo kwa Maktaba hiyo kutaongeza zaidi ufauru katika shule yake.
Furaha
Tonya Social Mobilizer wa Shirika la Room to Read Tanzania akiwa katika
Shule ya Sekondari Matibwa iliyopo Bagomoyo akielezea mradi wa Elimu
kwa mtoto wa Kike Tanzania unaoendeshwa na Shirika la Room to Read
ambapo moja ya mambo wanayo fundisha ni Life Skills ambapo lengo kubwa
ni kuwataka watoto waweze kujitambua.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Matibwa Ally Kilasama alisema kwamba mradi huo
umeweza kuwasaidia watoto wengi zaidi wa kike kuwepo katika shule hiyo,
katika mradi wa life skills alisema kuwa kwa sasa watoto wa kike
wameweze kujitambua zaidi na watoto wa kike wanafanya vizuri zaidi
kulipo wale wa kiume, pia kupitia mradi huo kutoka Room to Read wameweza
kupata vifaa ya Sayansi na vitabu vya kutosha kwa wanafunzi na kwa sasa
wanakarabati madarasa manne hii ikiwa ni juhudi za kutokomeza ujinga.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kingani wakiwa darasani wanamsikiliza mwalimu
Kutokana
na wanafunzi wakike kuelewa Elimu ya Life Skill wameweza kuwaburuza
wanafunzi wa kiume katika ufauru darasani ambapo katika Kidato cha tatu
Mchepuo wa Sayansi shule ya Sekondari Kingani Mwanafunzi mmoja tu mwanaume ndiye
ameweza kuingia katika kumi Bora ambapo hapa anaelezea jinsi kulivyo na
changamoto ya ushindani katika darasa hilo na kukili kuwa watoto wakike
wanaweza sana
Rose
Jeremiah Ngalya Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Mchepuo wa Sayansi aliye
ongoza na kushika nafasi ya kwanza akieleza namna ya Shirika la Room to
Read lilivyo wasaidia katika kuhakikisha wanapata Elimu Bora.
Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa
No comments:
Post a Comment