Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255629914471. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Na Godfriend Mbuya
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu haihusiki kumtafutia mnufaika wa mkopo
ajira badaya lake inahusika kumpatia mwanafunzi mkopo na akishamaliza muda wa
masomo atatakiwa kurejesha mkopo wake.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi
Msaidizi wa Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisobwa wakati akijibu maswali ya wananchi kupitia
mtandao wa Facebook.com/eatv.tv katika kipengele cha KIKAANGONI ambapo mgeni
hufika EATV na kujibu maswali ya hadhira kulingana na mambo mbalimbali
yanayohusu taasisi yake, au kazi yake.
“Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatoa mikopo suala la kutafuta ajira
halituhusu hivyo mnufaika yoyote asiwe na kigezo kwamba hajapata kazi , hiyo
siyo kazi yetu, kazi yetu ni kuwawezesha kupata elimu basi” Amesema Mwaisobwa.
Aidha Mwaisobwa amesema wanufaika wote ambao walipata mikopo wanatakiwa
kukatwa asilimia 8% ya pato la mwezi, na kama mtu anagfanya kazi binafsi na
hakatwi popote atatakiwa kutoa kiwango cha 120,000/= na kwa ambao wamenufaika na hawataki kuanza
kulipa mkopo watapigwa penati ya 10% ya mkopo kwa mwaka.
Pamoja na hayo Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imewataka walioomba mikopo
kuvuta subira kwani Bodi inasubiri majina kutoka Tume ya Vyuo Vikuu ili Bodi ya
Mikopo iweze kufahamu vyuo walivyopangiwa na kiwango cha ada ili haki iweze
kutendeka kwa waombaji.
No comments:
Post a Comment