Social Icons

Thursday, 1 September 2016

BODI YA MIKOPO KIKAANGONI

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255629914471. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako 

By Valentine Oforo, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Dodoma. Wabunge wameibana Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kwa kuongeza posho na kufikia jumla ya Sh1 bilioni katika kipindi kifupi kiasi ambacho hakilingani na kazi wanayoifanya.
Kwa kipindi kirefu, bodi hiyo imekuwa ikitupiwa lawama kwa kuchelewesha mikopo, kushindwa kukusanya fedha za wanafunzi waliokopa na kutoa mikopo kwa wanafunzi hewa.
Hivi karibuni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema bodi hiyo imetoa fedha za kujikimu na mafunzo kwa vitendo kwa zaidi ya wanafunzi hewa 1,000.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB, Abdul-Razaq Badru alijitetea mbele ya kamati hiyo akisema ni mgeni katika bodi hiyo na kwamba, wanaweka mikakati mizuri ya kurekebisha mambo hayo ili kuhakikisha inafanya kazi kwa weledi zaidi.
Wakizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) cha kukagua Ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2014/15 ya bodi hiyo, wabunge hao walisikitishwa na kitendo cha bodi hiyo kushindwa kukusanya zaidi ya Sh3 trilioni walizowakopesha wanafunzi mbalimbali tangu ianze kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
CHANZO GAZETI LA MWANANCHI

No comments: