Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255629914471. insta : @matukionawanavyuo Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Na: Lilian Lundo na Sheila Simba - MAELEZO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce
Ndalichako ametoa siku saba kuanzia Agosti 17, 2016 kwa vyuo vikuu
kurejesha fedha zilizopokea ambazo ni za wanafunzi ambao hawapo chuoni.
Prof. Ndalichako
ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na
waandishi wa habari juu ya taarifa la zoezi la uhakiki wa wanafunzi
wanufaika wa mikopo vyuo vya Elimu juu.
Prof. Ndalichako
amesema kuwa uhakiki wa wanafunzi hao umefanyika katika vyuo 31 kati ya
vyuo 81 vilivyopo nchini, Katika utafiti huo wanafunzi 2,192
wameshindwa kuhakiki majina yao, hivyo kushindwa kuthibitisha uwepo na
uhalali wa wanafunzi hao.
“Mikopo
ya Wanafunzi hao imesitishwa na kwa wale ambao ni wanafunzi halali
lakini walishindwa kujihakiki itabidi waombe tena mkopo,” alifafanua
Mhe. Ndalichako.
Ameendelea
kwa kusema kuwa, kwa mwaka wa fedha 2015/16 wanafunzi hao hewa
wameigharimu Serikali kiasi cha shilingi 3,857,754,460, kiasi ambacho
kinatakiwa kurejeshwa na vyuo ambavyo wanafunzi hao wamebainika.
Aidha, Prof. Ndalichako
amesema kuwa taarifa hiyo imekabidhiwa kwenye vyombo vya sheria ili
kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kufanya udanganyifu na kusababisha Serikali hasara ya mabilioni ya fedha.
Vile
vile Prof. Ndalichako amewataka wakuu wa vyuo kuweka mfumo wa kuhakiki
usahihi wa matokeo ya wanafunzi yanayotumwa Bodi ya Mikopo kutokana
na vyuo vingi kubainika kuwepo kwa udanganyifu mkubwa kwenye matokeo ya
wanafunzi ambao hawakufanya mtihani au waliofeli na kuandikiwa
wamefaulu ili waendelee kupata mikopo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment