Jonas Kamaleki, MAELEZO
Maandamano ya UKUTA hayawezekani kwani hii ni ndoto ya mchana na hayana msingi wowote wala tija kwa wahusika hata kwa Taifa.
Hayo yalisemwa na Muhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Benson Bana katika mahojiano maalum.
“Wanaotaka kuandamana
wanajidanganya na kuwalaghai wenzao kwani kufanya operesheni ni suala la
dola na si la mtu au kikundi cha watu, hivyo maandamano hayo
hayawezekani kabisa, alisema Prof. Bana.
Ameongeza kuwa
wanaojiita UKUTA ni kwamba Mhe. Rais John Pombe Magufuli amewanyima
ajenda kwani utendaji wake umezidi fahamu zao na kuwafanya waanze
kutapatapa wasijue nini la kufanya.
Prof. Bana amesema
kama viongozi wa UKUTA ni waungwana inabidi watamke wazi kuwa
wametafakari na kuona kuwa maandamano hayana maana hivyo wameamua
kuyasitisha nchi nzima.
Kuhusu utendaji wa
Serikali ya Awamu ya Tano, Prof. Bana alisema ni Serikali yenye maamuzi
ya uhakika na inayowajali watu wote bila kujali itikadi zao za vyama,
dini wala makabila hivyo inabidi watanzania waipende na kuiheshimu.
“Rais Magufuli
utendaji wake ni wa kuigwa na viongozi wengi Duniani kwani anafanya
maamuzi ya uhakika ikiwemo kukuza uchumi kwa kukusanya kodi na kuziba
mianya ya ubadhirifu wa mali ya umma, alisema Prof. Bana.
Pamoja na kuwa Rais
Magufuli amekuwa madarakani kwa kipindi kifupi, viashiria vyote
vinaonyesha kuwa ni kiongozi imara na shupavu kutokana na mambo makubwa
ambayo ameyafanya kwa kipindi hiki kifupi. Katika kipindi hiki
kumekuwepo na nidhamu katika utumishi wa umma, kodi inakusanywa kwa
kiwango kikubwa na elimu ya msingi inatolewa bure kama Ilani ya Uchaguzi
ya Chama Tawala inavyosema, alisema Prof. Bana.
Aidha, Prof Bana
amesema kuwa wanaomlaumu Mhe. Rais ni wale ambao hawajitambui na labda
wanaona mianya ya ubadhirifu anayoendelea kuiziba, wao wanakosa mapato,
vinginevyo Rais anafanya vizuri katika kuliongoza Taifa.
“Rais Magufuli yuko
sahihi kwa jinsi anavyosimamia vipaumbele vya Serikali ikiwemo elimu
bure, kukusanya kodi na kuzuia mianya ya rushwa pia dhamira ya kuifanya
Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda, alisema Prof. Bana.
Prof. Bana ameelezwa
kusikitishwa kwake na watu wanaomkosea Rais heshima na kumwita “Dikteta
Uchwara.”Amesema watu hawa inabidi wazalendo wakemee kabisa vitendo vya
namna hii ambavyo ni utovu wa nidhamu kwa kiongozi.
Akizungumzia uamzi wa
kuhamia Dodoma, Prof. Bana alisema kuwa ni uamzi wa busara kutekeleza
azma ya Serikali ya miaka takribani arobaini iliyopita. Hivyo kuhamia
Dodoma kutaufanya mji huo kuendelea zaidi kimiundombinu na kiuchumi.
Aliongeza kuwa mikoa
ya jirani nayo itanufaika kiuchumi kwani itakuwa karibu na makao makuu
ya nchi na pia kuhama huko kutatoa fursa kwa Dar es Salaam kukua zaidi
kibiashara.
Prof. Bana
ameitofautisha Serikali ya Awamu ya Tano na awamu nyingine nne
zilizopita kwa kutokuwa na kigugumizi katika kufanya maamuzi yake
ikiwemo hii ya kuhamia Dodoma, kuondoa wabadhirifu katika utumishi wa
umma na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na fedha hizo kutumika kwa
ajili ya miradi ya maendeleo kama afya, elimu na miundombinu.
No comments:
Post a Comment