Mkuu
wa Idara ya Uhandisi Mazingira (Environmental Engineering) Dr. Fredrick
Salukele akiwaelezea wanafunzi matumizi
ya vifaa mbalimbali vitumikavyo kwenye shughuli za ufundishaji, utafiti na
utoaji ushauri wa kitaalam, mfano wa vifaa hivyo ni Gaschromatograph
kinachoonekana kwenye picha.
Wanafunzi
wa Shule ya Mtakatifu Maximilian walipotemblea Maabara ya Sayansi ya Mazingira
na Tekinolojia ya Chuo Kikuu Ardhi. Maabara hiyo hutumika kwa ajili ya shughuli
za Ufundishaji, Utafiti na Uhauri wa kitaalamu katika fani ya Sayansi ya Mazingira.
Wanafunzi
wakiangalia kwa makini baadhi ya kazi za ubunifu majengo zilizo fanywa na
wanafunzi wa Skuli ya Ubunifu Majengo wa Chuo Kikuu Ardhi. Kubuni aina
mbalimbali za majengo ni moja kati ya mahitaji kwenye mtaala wa kufundishia
program ya Usanifu Majengo ya Chuo Kikuu Ardhi
Mtaalam
kutoka Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Pius Lugomela
(mwenye shati la bluu), akitoa malezo kuhusu vifaa mbalimbali vya upimaji
ramani vilivyoko kwenye maabara ya Skuli iyo.Vifaa kwenye maabara hiyo pia hutumika
kwa ajili ya shuguli za ufundishaji, utafiti na ushauri wa kitaalamu kwenye
maenneo ya upimaji ardhi na ramani.
Na. Hadija Maulid - Chuo Kikuu Ardhi.
Chuo
Kikuu Ardhi kimetoa wito kwa wanafunzi wanaosoma darasa la saba kote nchini kufanya
bidii katika masomo ya Sayansi na Hisabati ili waweze kujenga msingi imara na kuandaa
mazingira ya kujiunga na fani za Sayansi katika elimu ya Sekondari na vyuo
vikuu.
Wito
huo huo umetolewa leo jijini Dar es
salaam na baadhi ya wataalamu wa Chuo hicho mara baada ya kuwapokea wanafuzi 84
wa Shule ya Msingi ya Mtakatifu Maximilian waliotembelea maeneo mbalimbali ya chuo
hicho kwa lengo la kujifunza majukumu ya chuo hicho na elimu inayotolewa.
Wakiwa
chuoni hapo wanafunzi hao wamepata fursa ya kuitembelea Skuli ya Sayansi ya
Mazingira na Teknolojia (Environmental Science and Technology) Skuli ya Ubunifu
Majengo (School of Architecture and Design) na Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki na
Tekinolojia (School of Geospatial Sciences and Technology).
Aidha,
Wanafunzi hao walipata fursa ya kuuliza maswali mbali mbali kwa wataalamu.
Ziara
hiyo imelenga kuwahamasisha wanafunzi kufanya
vizuri katika masomo ya Sayansi ili waweze kupata alama za juu zitakazowawezesha
kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita na kisha kujiunga na Chuo kikuu
Ardhi ili baadaye wawe wataalamu katika fani mbalimbali za Ardhi na Mazingira.
No comments:
Post a Comment