Social Icons

Friday, 10 June 2016

WAHITIMU WA USCF - TAASISI YA UHASIBU TANZANIA WATAKIWA KUWA WAADILIFU MAKAZINI

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 

Wanafunzi wametakiwa kuwa waadilifu pindi wanapomaliza chuo na kwenda kuingia makazini. Kauli hiyo ameitoa Mwenyekiti wa bodi ya Ushauri TAREA, Godwin Msigwa (pichani) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikiristo wa vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend iliyopita. Msingwa alisema ni vyema vijana wakatambua kuwa maisha mazuri ni yake ya kufanya kazi kwa uadilifu na kuacha ujanja ujanja katika kazi. "Leo mnaenda mtaani mtapata kazi ninawaomba mkafanye kazi kwa uadilifu, mfano wewe ukipata kazi ya kusimamia manunuzi ya dawa muendele ukanunue dawa zenye ubora maana usipofaya hivyo utasababisha vifo vya watu na hiyo dhambi si ndogo, Muogopeni Mungu,' Alisema Msigwa. Aliongeza kuwa wakati umefika kwa watanzania wakaonyesha uzalendo kwa mambo yao wenyewe, wasingoje mpaka wasukumwe katika kufanya kazi kwa bidii. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Mchungaji wa KKKT akitoa neno wakati wa mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikiristo wa vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend iliyopita.
Wahitimu wakifuatilia neno kutoka kwa mchungaji wakati wa mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikiristo wa vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend iliyopita.
Katika neno alililolitoa mchungaji huyu aliwaasa wahitimu kuwa na hofu ya Mungu pindi wanapopewa majukumu ya kazi.
Mgeni rasmi mwenyekiti wa bodi ya Ushauri TAREA, Godwin Msigwa (wa tatu toka kushoto) akiserebuka na mchungaji wa KKKT pamoja na wageni waalikwa.
Wahitimu wakijimwaga.
 Mchungani akiwaombea wanafunzi wakafanye vyema katika mitihani yao wakati wa mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikristo wa vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika

No comments: