Social Icons

Friday, 24 June 2016

TANZANIA BADO INAHITAJI WATAALAM WALIOBOBEA KATIKA BIASHARA YA KIMATAIFA

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 
 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema wakati akifungua mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili program mpya mbili za masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili katika Biashara ya Kimataifa  na Ugavi, Usimamizi mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.
Mmoja wa washiriki wa Mkutano huo akichangia wakati wa Mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini majadiliano kuhusu program mpya mbili za masomo katika ngazi ya
Shahada ya Uzamili katika Biashara ya Kimataifa  na Ugavi, Usimamizi wa mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na CBE.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema akiwa katika picha ya pamoja  na wadau mbalimbali waliohudhuria katika chuo hicho kujadili program mpya mbili za masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili katika
Biashara ya Kimataifa  na Ugavi, Usimamizi mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.
 
Na. Aron Msigwa Dar es salasam.
 
Tanzania bado inahitaji wataalam waliobobea katika Biashara ya Kimataifa na wale wanaosimamia mfumo wa uzalishaji, usambazaji na utunzaji  wa bidhaa mbalimbali hususan mazao ya chakula ili kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo gharama kubwa ya uagizaji, utunzaji, usambazaji na hasara ya kuharibika  kwa mazao inayowakumba wafanyabiashara walio wengi kabla ya kufikisha bidhaa zao kwa walaji.
 Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema wakati akifungua mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili program mpya mbili za masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili (Masters)katika Biashara ya Kimataifa  na Ugavi, Usimamizi wa mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.
 Amesema ili kukabiliana na changamoto hizo zinazowakumba wakulima na wafanyabiashara walio wengi hasa wale wa matunda ambao hupoteza karibu asilimia 40 ya mazao yao, lazima hatua madhubuti zichukuliwe kwa kuwajengea
uwezo wa kitaalamu vijana wa Kitanzania ambao wataweza kukabiliana na changamoto ya wakulima kupata hasara kwa kuhakikisha mazao yanayotoka kwenye maeneo ya uzalishaji yanafika yakiwa salama.
Leo tuna mkutano wa wadau kwa sababu CBE tuko katika hatua za mwisho za mchakato wa kuanzisha Programu mpya za Shahada za uzamili katika katika masuala ya Ugavi (Procurement and Supply Chain Management) pia Shahada ya
Uzamili katika Biashara ya Kimataifa (International Business Management) ili tuweze kutoa mafunzo yatakayowasaidia watanzania
’’
Amebainisha kuwa mazao kama matunda mara nyingi yamekuwa yakiharibika katika hatua ya kuvunwa, kusafirishwa na
kuhifadhiwa jambo linalowasababishia hasara wakulima pamoja na wasafirishaji kwa kuwa hawana ujuzi na utalaam wa usimamizi wa bidhaa na mazao yao.
Aidha, ameongeza kuwa asilimia 40 ya gharama hizo hutumika katika masuala ya usafirishaji na  ufuatiliaji wa bidhaa husika kuifikisha kwa mlaji na kusisitiza kwamba gharama hizo husababishwa na mfumo mzima unaopaswa kupitiwa kabla ya kuifikisha bidhaa husika sokoni jambo ambalo lingerekebishwa kwa kuwa na wataalam wa kutosha kusimamia sekta hiyo.

No comments: