Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha 34 cha Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifurahia jambo
na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ndani ya
Ukumbi wa Bunge kabla ya kuanza kwa kikao cha 34 cha Mkutano wa 3 wa Bunge mjini
Dodoma.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi na Sekondari Moga iliyoko jijini Dar es salaam wakifuatilia
shughuli za kikao cha 34 cha Bunge mjini Dodoma. Wanafunzi 90 wa shule hiyo
wamelitembelea Bunge hilio kujifunza namna linavyoendeshwa.
Baadhi ya
Mawaziri na Wabunge wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 34
mjini Dodoma.
Naibu Waziri
wa Malisili na Utalii Mhe. Ramo Makani akijibu maswali ya Wabunge
yaliyoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa kipindi cha Maswali na majibu leo,
Dodoma.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Muhagama akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya
utendaji wa Serikali ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 leo mjini Dodoma. Wizara
hiyo inaliomba Bunge lipitishe kiasi cha shilingi Trilioni 8.7 kwa ajiri ya
matumizi ya kawaida na matumizi mengine.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji
wakiandika maoni ya Wabunge waliokuwa wakichangia Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara Fedha na Mipango kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 leo mjini
Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kulia)
akimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina nje ya Ukumbi wa Bunge leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kushoto)
akisalimiana na Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto nje ya Ukumbi wa Bunge,
Dodoma.
Baadhi
ya Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Moga iliyoko jijini Dar
es salaam wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya
kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge kufuatilia shughuli za kikao cha 34.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kulia)
kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma.
Na. Aron Msigwa-
DODOMA.
Serikali imesema kuwa
itaendelea kuboresha maslahi ya askari wa Jeshi la Polisi na kuwajengea nyumba
za kisasa za kuishi ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina wakati
akijibu maswali ya wabunge kuhusu mkakati wa Serikali wa kuboresha maslahi ya
Askari wa Jeshi hilo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Bungeni
mjini Dodoma leo
Amesema kuwa Serikali
katika mwaka wa fedha 2016/2017 itatekeleza Mpango kabambe wa ujenzi wa nyumba za
Polisi 4136 ambao utakwenda sambamba na ujenzi wa vituo vya Polisi.
Amesema Serikali imechukua
hatua za haraka kulishughulikia suala la ukosefu wa nyumba za askari hao katika
maeneo mbalimbali nchini ili kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yenye
ukosefu wa nyumba hizo.
Amelieleza Bunge kuwa
Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa maslahi ya Askari
Polisi yanaimarishwa ikiwemo malipo ya Posho ya pango kwa askari wasio na
nyumba ambayo ni asilimia 15 ya mishahara yao ili waweze kulipia gharama hizo.
Ameongeza kuwa askari wenye utalaam maalum wakiwemo madereva
na madaktari wamekuwa wakilipwa posho ya asilimia 15 ya mishahara yao na kuongeza
kuwa askari wanaoajiriwa katika ajira mpya kama madaktari wamekuwa wakilipwa mishahara
sawa na madaktari wengine bila kujali vyeo vyao.
“Serikali tumefanya
jitihada kubwa sana kuboresha maslahi ya askari wetu, kama Serikali tumetoa
posho za nyumba, posho za utalaam maalum kwa askari wote ambayo ni asilimia 15
ya mshahara wa kila Polisi hii yote ni kuwafanya askari wetu waweze kumudu
gharama za maisha” Amesisitiza Mhe. Mpina.
Ameeleza
kuwa kwa askari wanaofanya kazi katika mazingira magumu wakiwemo wa Kikosi cha
Kutuliza Ghasia (FFU) wamekuwa wakipewa posho ya kufanya kazi katika mazingira
magumu (Hardship allowance) kiasi cha shilingi laki moja (100,000) kila mwezi.
Mhe.
Mpina amebainisha kuwa askari wote wanaohitimu mafunzo yao wamekuwa wakikatiwa
Bima ya Afya kwa asilimia 100 na Serikali pamoja na udhamini wa mikopo
mbalimbali katika taasisi za kifedha ili waweze kupewa mikopo na taasisi hizo.
Aidha,
amesisitiza kuwa serikali imewapandishia kiwango cha Posho ya katikati ya mwezi
(Ration Allowance) kutoka shilingi 180,000 za awali hadi 300,000 ambazo
wanalipwa kwa sasa nchi nzima.
Katika
hatua nyingine Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imetoa ufafanuzi
kuhusu vijana wa kidato cha nne kutochukuliwa kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa hatua ya kuwachukua vijana wote
wanaomaliza kidato cha nne kwa sasa haiwezekani kutokana na uwezo mdogo wa
kifedha wa Serikali.
Amesema
kuwa uwezo wa JKT kuchukua vijana wa kujitolea kwa sasa ni 5000 hadi 7000 kwa
mwaka kulingana na bajeti inayotolewa na kuongeza kuwa mpango wa Serikali ni
kuendelea kutenga fedha na kujenga kambi zaidi za mafunzo ili kuwawezesha
vijana wengi kujiunga na mafunzo hayo kulingana
na upatikanaji wa fedha.
Kwa
upande wa wahitimu wa kidato cha sita wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa
Sheria Mhe. Mwinyi amesema Serikali imewachukua vijana 14,000 na inaendelea
kujenga uwezo wa ndani wa kuchukua vijana wengi zaidi.
Amesema
Serikali inakusudia kujenga majengo ndani ya makambi ili kuwezesha vijana wote
wanaohitimu kidato cha sita kupitia JKT kabla ya kujiunga na vyuo mbalimbali
hapa nchini.
Aidha,
Amefafanua kuwa kwa wale wanaojiunga na JKT kwa kujitolea ambao idadi yao
inafikia 5000 sio wote wanaopata nafasi ya kuajiriwa katika vyombo vya Ulinzi
na Usalama na kuongeza kuwa ni asilimia 71 ndio hupata ajira kwenye vyombo
hivyo huku waliobaki wakilazimika kurudi nyumbani.
Amebainisha
kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaangalia utaratibu wa kuwawezesha
vijana hao ili wanaporudi uraiani waweze kupatiwa mitaji ya kuwawezesha kujiajiri
wenyewe.
No comments:
Post a Comment