Na Daudi
Manongi-MAELEZO
UONGOZI Chuo Kikuu
cha Dar es salam unatarajia kununua taa za dharura 12 kwa ajili ya kukabiliana
na tatizo la giza katika Hosteli ya Mabibo.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar es salaam na Naibu Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
anaeshughulikia masuala ya Utawala Prof.David Alfred Mfinanga wakati wa
mahojiano na Idara ya Habari.
Alisema kuwa tatizo
la giza nene katika eneo hilo la lango kuu la kuingia Hostel za mabibo mpaka
eneo lile la maegesho ya magari lipo mbioni kupatiwa ufumbuzi baada ya taratibu
za ununuzi kukamilika.
Alisema kuwa
kukamilika kwa uwekaji wa taa hizo za dharura zitapunguza kabisa tatizo hilo.
Aidha, Prof.David
Alfred Mfinanga alisema kuwa katika
mpango wa muda mrefu wa kutatua tatizo hizo uongozi wa UDSM unatarajia kuweka
umeme wa jua ambao utapunguza gharama za kulipia umeme na hivyo kuwa na umeme
wa uhakika.
Hostel hizo za kisasa
zilizojengwa miaka michache iliyopita na Shirika la Hifadhi za Jamii(NSSF)
zimesaidia kupunguza tatizo la makazi lililopo kampasi kuu ya Chuo
kikuu(mlimani) lakini kasoro hizi za
kukosa umeme zinahatarisha eneo hilo kugeuka kuwa la ubakaji na hata ukabaji
kwa wanafunzi na wageni.
No comments:
Post a Comment