Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dk...
Naibu Waziri akiangalia vitabu vilivyopo kwenye Maktaba ya Chuo hicho |
Naibu Waziri akiwaeleza jambo uongozi wa chuo hicho. |
Naibu Waziri akikagua Darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Chuo cha Diplomasia |
Dkt. Suzana Kolimba akizungumza na uongozi wa Chuo cha Diplomasia mara baada ya kumaliza kuzungukia eneo la Chuo cha Diplomasia |
Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia naye akizungumza wakati Naibu Waziri alipotembelea Chuo hicho |
Naye Mkurugenzi wa Taaluma, Dkt. Watengere Kitojo akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Naibu Waziri |
Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu Chuoni hapo Dkt. Charles Bekon akionesha Mpango Mkakati wa Chuo cha Diplomasia ikiwemo mfano wa michoro ya majengo ya Chuo. |
Naibu Waziri Dkt. Susan Kolimba akitazama sampuli ya michoro ya majengo yanayotarajiwa kujengwa Chuoni hapo |
Dkt. Susan akisalimiana na Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia mara baada ya kuwasili Chuoni hapo. |
Picha na Reginald Philip
----
----
Naibu Waziri Dkt. Kolimba aeleza nia ya Wizara katika kuendeleza Chuo cha Diplomasia
Wizara
ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
imejipanga kuhakikisha Chuo cha Diplomasia kinaboresha huduma zake za
utoaji elimu na mafunzo ya masuala ya Diplomasia ili kukidhi mahitaji ya
Watanzania katika taaluma hiyo.
Hayo
yalibainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba alipofanya
ziara katika Chuo hicho kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam ambacho
ni moja ya Taasisi zilizo chini ya Wizara.
Mhe.
Kolimba alisema kwamba Chuo cha Diplomasia ambacho kilianzishwa kwa
ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Msumbiji ni miongoni mwa vyuo
vilivyojipatia sifa kubwa ndani na nje ya nchi kwa kutoa mafunzo
katika masuala ya Diplomasia na hivyo Wizara haina budi kuhakikisha
inaendelea kukiboresha ili kuhakikisha kinakidhi viwango vya kitaifa na
kimataifa.
Mhe.
Dkt. Susan alisema kuwa, miongoni mwa masuala yanayotakiwa kufanyiwa
kazi katika maboresho hayo ni pamoja na miundombinu ya Chuo kwa maana ya
kuongeza majengo, vifaa vya kisasa vya kufundishia, maabara za kisasa
za lugha, maktaba na kuongeza Wakufunzi.
Aidha,
Mhe. Kolimba aliueleza Uongozi wa Chuo hicho kuwa ni vema vipaumbele
katika kukiletea chuo maendeleo vikaainishwa ikiwa ni pamoja na
kuonyesha mikakati ya kila changamoto ili kupata suluhisho la haraka la
changamoto hizo.
“Ninawapongeza
kwa kazi nzuri mnayofanya na tunaahidi kuwa pamoja nanyi wakati wote
ili kuhakikisha Chuo chetu kinafikia viwango vinavyostahili” alisema
Mhe. Kolimba.
Vilevile
alieleza kuwa ni vema Chuo kikaimarisha ushirikiano na Vyuo vingine vya
ndani na nje kwa kuainisha maeneo muhimu ya ushirikiano yenye faida kwa
pande zote. Pia alikitaka Chuo kuwa na mikakati itakayokiwezesha Chuo
hicho kuweza kujiendesha kibiashara kama vyuo vingine nchini na kuacha utegemezi mkubwa katika bajeti ya Serikali.
Awali
akimkaribisha Naibu Waziri Chuoni hapo, Mkurugenzi wa Chuo hicho,
Balozi Mohammed Maundi alisema kuwa Chuo hicho kinaendelea kuboresha
maeneo mbalimbali ya Chuo hicho ikiwemo kuanzishwa kwa Kozi ya Shahada
mwaka 2015 na tayari chuo kimepata michoro ya majengo kwa Chuo kipya
wanachotarajia kukijenga na sasa kinachohitajika ni fedha ili
kukamilisha mpango huo ambao kwa kiasi kikubwa utamaliza changamoto
zinazokikabili Chuo.
Chuo
cha Diplomasia (CFR) ni chuo kilichoanzishwa kwa ushirikiano baina ya
Serikali ya Tanzania na Msumbiji mwaka 1978. Chuo kimekuwa kikitoa elimu
katika ngazi ya Cheti, Diploma, Shahada na Shahada ya Juu.
No comments:
Post a Comment