Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana pamoja na
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al –
Sumait wakiingia kwenye uwanja kwa ajili ya Mahfali ya 15 ya chuo hicho
hapo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ambae
alimuwakilisha Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein kwenye Mahafali
hayo ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Hicho Dr. Abdulrahman Al - Muhailan
na kushoto ya Balozi Seif ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Profesa
Hamed Rashid Hikmany.
Wahitimu
wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait
wakiingia kwa maandamano kwenye uwanja kwa ajili ya kupewa stashahada
zao.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr.
Abdulrahman Al – Sumait, Dr. Abdulrahman Al – Muhailan akitoa salamu
kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho hapo chukwani.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment