Social Icons

Saturday 12 December 2015

Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi waliofanya Vizuri wanyakua Tuzo mbalimbali

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idrisa Mshoro akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa nne aliyefanya vizuri katika masomo yake kwa mwaka 2014/2015  wakati wa leo jijini Dar es salaam.
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia masuala ya Taaluma wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Gabriel Kassenga akizungumza na wanafunzi na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa Tuzo kwa wahitimu wa chuo hicho waliofanya vizuri leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, wawakilishi wa Makampuni na Taasisi mbalimbali waliochangia tuzo mbalimbali na Wahitimu wa miaka ya nyuma wa Chuo hicho wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla fupi ya utoaji wa Tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri leo jijini Dar es salaam.
  Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi waliofanya Vizuri waendelea kupokea tuzo zao. Takribani wanafunzi 126 wamepata Tuzo na zawadi mbalimbali wakiwemo wanafunzi kike 61 waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi.
 Wanafunzi na Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo
 Mwanafunzi Bora wa Kike wa Chuo Kikuu cha Ardhi katika fani ya Upimaji wa Ardhi ( Geomatics) Bi. Lilian Kato akipokea zawadi yake ya mashine ya kupimia Ardhi (Total Station) yenye thamani ya shilingi milioni 15 aliyozawadiwa na Kampuni ya High Tech Systems kwa kuwa mwanafunzi bora wa kike wa mwaka wa nne kwa mwaka 2014/2015

No comments: