Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Kuna makadirio ya watanzania milioni 23 kwenye soko la ajira.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Alisema kwa sasa kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa ajira nchini
kunakosababishwa na ukosefu wa ujuzi wa maendeleo, huku zaidi ya
watafuta ajira 800,000 kutoka nje ya nchi wakiingia nchini kutafuta
ajira kila mwaka.
Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya
kuandaa mkakati wa kitaifa wa kujenga na kuimarisha stadi za kazi katika
sekta zinazochochea ukuaji uchumi , iliyowakutanisha baadhi ya makatibu
wakuu nchini.
Alisema kwa sasa nchi inahitaji mfumo wa elimu ambao utawasaidia
vijana kupata ajira kwa urahisi kwa kuwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa
vijana linazidi kukua siku hadi siku na kuhatarisha uchumi wa nchi.
Aliongeza kuwa ingawa uchumi unakua kwa wastani wa asilimia sita
hadi saba kwa mwaka tangu miaka kumi iliyopita, lakini ukuaji huo
haujasaidia upatikanaji wa ajira ya uwakika kwa vijana wanaomaliza
masomo vyuoni.
“Leo kuna makadirio ya Watanzania milioni 23 kwenye soko la ajira,
na idadi hiyo inakisiwa kuongeza hadi kufikia milioni 45 ifikapo mwaka
2030, na ongezeko la watu linakua kwa kasi kwa milioni 1.2 kwa mwaka,
hivyo tusipokuwa makini tutatengeneza kizazi kisicho kuwa na elimu,”
alisema Sefue.
Aliongeza kuwa taasisi za elimu nchini hususani vyuo vikuu
wanawapatia wanafunzi ujuzi ambao hauendani na soko la ajira ama elimu
ambao haiendani na nini soko la ajira duniani linahitaji.
Alisema taasisi za elimu zinapaswa kuboresha masomo kwa wanafunzi
wao ambayo yataendana na soko la ajira pamoja na kuinua uchumi wa nchi
utakaosaidia kuwavutia wawekezaji kwa wingi
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF),
Godfrey Simbeye, alisema Serikali na sekta binafsi zinapaswa kufanya
kazi kwa pamoja ili kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana kwa
kutengeneza sera madhubuti zitakazo okoa tatizo hilo.
Alisema kwa kuwapo kwa sera ya maendeleo ya ujuzi katika elimu
kutasaidia kuwaongezea vijana ujuzi wa kufanya kazi pindi wawapo katika
masomo na kuutumia ujuzi huo watakapokuwa wakitafuta ajira ama
wakishaajiriwa.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment