Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.
wataalamu wa kada hiyo kwa lengo la kupunguza ama kumaliza vifo vya mama na mtoto.
Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga
Profesa Richard Lema, kwenye mahafali ya saba ya stashahada na ya pili
ya cheti kwa wahitimu wa uuguzi na ukunga toka chuo cha Massana, jijini
Dar es Salaam.
Profesa Lema alisema iwapo vyuo binafsi vitapatiwa ruzuku na
serikali kama inavyofanyika kwa vyuo vyinavyomilikiwa na misheni, kada
ya uuguzi na ukunga itapata watumishi wengi, hivyo kuisadia serikali
katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto nchini.
“Ni dhahiri hatuwezi kupunguza vifo vya akina mama na watoto bila
ya wakunga wa kutosha kwani hawa ndio wadau muhimu wa kupunguza vifo vya
akina mama na vitoto vichanga, na muhimili wa kutekeleza malengo ya
namba nne na tano ya Milenia,” alisema.
Alisema tatizo linalovikumba vyuo vya ukunga na uuguzi vya watu
binafsi kama hicho cha Massana, ni lile la wanafunzi wa fani
hiyo kushindwa kuendelea kutokana na tatizo la ada, pale wafadhili wao
wanapojitoa kutokana na sababu mbalimbali.
Alisema tatizo hilo linaweza kutatuliwa na serikali kwa njia
tofauti, ikiwa ni pamoja na kuwaingiza walimu wa vyuo binafsi vya
uuguzi na ukunga kwenye mpango wa mkataba na Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii.
“Na hili linawezekana tukiwa kama wadau wa serikali, kwa sababu
wahitimu wetu huajiriwa na wizara na kupangiwa kufanya kazi katika
maeneo karibu yote nchini,” alisema.
Naye mgeni rasmi katika mahafali hayo, Profesa Paulina Meela,
aliwataka wahitimu hao wakafanye kazi kwa kuzingatia miiko na maadili
kama walivyofundishwa.
Jumla ya wanafunzi 23 wa Stashahada ya uuguzi na ukunga inayochukua
miaka mitatu na wanafunzi 17 wa cheti cha miaka miwili, walihitimu
mafunzo hayo.
CHANZO:
NIPASHE
Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
No comments:
Post a Comment