Wewe ni Mwanachuo? Tuwasiliane kwa namba 0654221465
Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
SERIKALI imesema kuwa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es salaam utagharimu kiasi cha Dola za kimarekani Milioni 61.
Katika mradi huo serikali yTanzania imechangia dola za kimarekani milioni 18 na serikali ya Jamhuri ya Korea imetoa mkopo wa dola za kimarekani milioni 43 ili kufanikisha ujenzi wa chuo hicho katika eneo la Mlonganzila jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kukamilisha ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho jana jijini Dar es salaam Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa alisema kuwa mradi huo na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwakani.
“Tumejipanga vizuri kujenga Chuo hiki cha Tiba ambacho kitakua mji wa tiba hapa nchini, sisi kama serikali tumeiona changamoto ya wataalam wa afya nchini na kuona ni vyema kujenga chuo cha kisasa kitakachokua na uwezo wa kupokea zaidi ya wanafunzi 15,000 kwa mwaka watakaosaidia kuondoa tatizo la wataalamu wa afya.” alisema Dkt.Kawambwa.
Dkt. Kawambwa alisema kuwa mbali na ujenzi wa chuo hicho, serikali itajenga hospitali nyingine ya Muhimbili ambayo ujenzi wake utamalizika sambamba na ujenzi wa chuo hicho ili kuwawezeha wananchi kupata huduma bora za afya.
Alibainisha kuwa hospitali hiyo pindi itakapokamilika itakuwa kubwa zaidi na yenye vifaa vya kisasa itakayosaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa uliopo katika hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na kuwasaidia wanafunzi kupata sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Tiba Muhimbili Prof. Ephata Kaaya alisema mradi huo umegawanyika katika awamu mbili, awamu ya kwanza ikihusisha ujenzi wa chuo cha tiba na Hospitali ya kisasa ya muhimbili na awamu ya pili itakuwa ujenzi wa hospitali kubwa ya kutibu magonjwa ya Moyo na mishipa ya fahamu.
“ Tayari Benki ya Maendeleo Afrika imetoa kiasi cha zaidi ya dola za kimarekani milioni 9 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo na hospitali ya kimataifa ya magonjwa ya moyo na mishipa ya fahamu itakayokuwa na ubora wa hali ya juu katika nchi za Afrika Mashariki” alisisitiza Prof.Kaaya .
Aliongeza kuwa gharama ya vifaa tiba ikiwemo vya uchunguzi na upasuaji utagharimu zaidi ya dola za kimarekani Milioni 27 na kueleza kuwa mkandarasi wa kufunga vifaa tiba vya mradi huo ameshapatikana na anatarajia kuanza kufanya kazi hiyo hivi karibuni.