Social Icons

Thursday 6 November 2014

SUA kutumia shilingi milioni 65 kushawishi matumizi ya Mtama.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha kilimo Sokoine, Profesa Joseph Phillip Hella, akitoa mada yake ya uongezaji wa uzalishaji wa Mtama katika wilaya tisa zinazokabiliwa na ukame hapa nchini.
Afisa kilimo umwangiliaji na ushirika wilaya ya Singida, Abel Mngale, akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya uhabarisho juu ya kuongeza uzalishaji wa zao la Mtama kwenye wilaya tisa zinazokabiliwa na ukame nchini.Kulia ni mhadhiri wa chuo kikuu kilimo cha Sokoine mjini Morogoro, Profesa Joseph Philip Hella na kushoto ni mhadhiri chuo kikuu kilimo Sokoine, Dk.Mafuru.

Baadhi ya maafisa ugani mkoa wa Singida, waliohudhuria semina iliyohusu uongezaji wa uzalishaji wa zao la mtama kwenye wilaya tisa zinazokabiliwa na ukame hapa nchini.

Mhadhiri wa chuo kikuu kilimo Sokoine Morogoro,Profesa Joseph Phillip Hella (wa nne kushoto mwenye miwani waliosimama) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanasemina baadhi ya maafisa ugani mkoa wa Singida.Maafisa hayo walihudhuria semina iliyohusu kuongeza uzalishaji wa zao la Mtama.

CHUO kikuu cha kilimo cha Sokoine Morogoro, kinatarajia kutumia zaidi ya shilingi 65 milioni kugharamia mradi wa kuongeza matumizi ya zao la Mtama,ili kukuza soko la zao hilo linalostahimili ukame.

Imedaiwa kwamba soko la Mtama likikua kutokana na kuongezeka kwa matumizi, wakulima wataongeza uzalishaji zaidi ili kukidhi mahitaji ya soko.

Hayo yamesemwa na Mhadhiri wa chuo hicho Profesa Joseph Phillip Hella,wakati akizungumza na MOblog  juu ya mradi huo wenye lengo la kupanua wigo wa matumizi yam tama katika wilaya tisa nchini.


Alisema uzalishaji mdogo uliopo hivi sasa unachangiwa na zao la Mtama kukosa  soko la uhakika,na hali hiyo inatoka na  matumizi yake kuwa  madogo mno.

Akifafanua,Profesa Hella alisema zao la Mtama limekuwa likitumiwa kwa ajili ya kutengneza uji,kupikia ugali na kutengenezea pombe ya kienyeji tu.

“Kupitia mradi wa SMU (sorghum for multiple use), tunatarajia kupanua wigo wa matumizi ya  mtama ambayo ni kutengenezea chakula cha mifugo, mikate, keki na pia utumike kutengenezea bia.Kwa njia hii wakulima wataongeza uzalishaji kwa sababu soko litakuwa na wateja wengi”,alisema.

Akifafanua zaidi,Profesa Hella,alisema pia zao la Mtama ni lishe bora kwa wagonjwa wa kisukari,kwa hali hiyo,upo umuhimu mkubwa wa kuongeza uzalishaji wake, ili wakulima waweze kujitosheleza kwa chakula na kujikomboa kiuchumi.

Wilaya zitakazofaidika na mradi huo wa miaka mitatu,ni Kongwa,Kondoa,Iramba,Singida,Seregenti,Same,Mwanga,Moshi na Rombo.


Kwa mujibu wa Profesa Hella,mradi huo unafadhiliwa na shirika la IFAD na jumuiya ya chi za ulaya.Unatekelezwa katika nchi za Tanzania na Kenya.Tanzania ni ya tatu katika bara la Afrika ikizifuatia Sudan na Ethiopia.
Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.

No comments: