|
Jamaa walivyo matapeli wametumia jina la Mh. Sumae Waziri mkuu mstaafu kuwa ndiyo alizinduo chuo hicho kumbe ni uongo mtupu |
|
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Bi Quip Mbeyela aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Norman Sigala akitoa tamko la kufunga chuo hicho |
|
Kulia ni Richard Mchomvu mkuu wa Polisi wilaya ya Mbeya akiwa na jalada la uchunguzi kuhusiana na chuo hicho |
|
Baadhi ya wanafunzi wakiwa hawaamini tamko lililotolewa na Selikari juu ya kufungwa chuo chao |
|
Hakika ilikuwa huzuni kubwa kwa wanachuo hao |
|
Wakazi wa ilemi wakiomboleza na wanachuo hao |
|
Serikal
imekifunga chuo cha Kilimo na Mifugo cha Nice Dream kilichopo mtaa wa Mapelele
Kata ya Ilemi Jijini na kuwataka wanachuo wa chuo hicho kuondoka chuoni hapo
baada ya siku tatu.
Agizo
hilo lilitolewa na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Bi Quip Mbeyela
aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Norman Sigala na kwamba
Serikali itagharamia chakula kwa siku tatu ambapo Serikali ilikabidhi shilingi
laki tatu kwa Mtendaji Kata Bi Gladness Sapuka kwa ajili ya kununua chakula kwa
wanachuo 48 waliokuwa wakisoma katika chuo hicho ambacho hakina usajili kutoka
Baraza la Vyuo(NACTE).
Tamko
hilo lilamsha kilio chuoni hapo kutoka kwa wanachuo na wakazi wa Ilemi kutokana
na wanachuo hao kutakiwa kuwasiliana na wazazi wao na walezi ili watumiwe nauli
za kuwasafirisha makwao na wengi wao wakitokea mkoa wa Kagera na Mara na kwamba
wanachuo hao wamekwisha lipa kila mmoja zaidi ya shilingi laki tano na elfu
hasini.
Mbali
ya chuo hicho kutosajiliwa na NACTE pia mmiliki wake hafahamiki vema na jalada
la uchunguzi ili akamatwe kujibu tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu kwa kutumia kivuli cha chuo na kuwatapeli wanachuo 48 waliokuwa na
nia ya kusomea taaluma ya kilimo.
Kauli
hiyo ilikuwa mwiba kwa wanachuo hao pale Kaimu Katibu Tawala aliposema kwamba
Serikali haina chuo cha kuwapeleka kwa kuwa hakuna nafasi katka Vyuo vya Kilimo
Mkoani Mbeya na muda wa usajili wa wanavyuo vya kilimo umemalizika.
Kaimu
Katibu Tawala aliambatana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbeya Richard Mchumvu
ambaye alisema kuwa Jeshi la Polisi linamtafuta mtuhumiwa na kwamba pindi
atakapopatikana atafikishwa mahamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kwa
upande wa wakazi wa Ilemi wameiomba Serikal kuangalia upya suala hilo kwa kuwa
mtuhumiwa hajakamatwa hivyo serikali iwasaidie usafiri wa kuwaridisha wanachuo
hao makwao ili kuwapunguzia makali kutokana na umbali wanaotoka.
Wazo
hilo liliungwa mkono na Diwani wa Kata ya Ilemi Furaha Mwandalima ambaye
alisema serikali ione hilo kama janga la moto au mafuriko il kuwasaidia
kuwasafirisha makwao kwani wengi wa wanachuo hawana uwezo wa kupata nauli ya
kuwafikisha makwao ambapo mwanachuo mmoja anahitaji kutumia zaidi ta shilingi
laki moja na zaidi ya shilingi milioni sita zinahitajika kuwafikisha makwao.
Pamoja na kauli ya Serikali kutoa tamko
wakazi wa Ilemi walibaki ili kujadiliana mustakabali wa wa wanachuo hao
kutokana na wengi kutoka katika familia duni na wengi kuonekana kukata tamaa ya
kuishi kwa kile walichodai kuwa mmoja wao alikuwa ni pacha na mwenzake ambapo
nduguye aliozwa ndipo zikapatikana fedha za karo.
Na Tone Multimedia
|
Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
No comments:
Post a Comment