Taasisi
ya RafikiElimu FOUNDATION kupitia MRADI WA ELIMU YA
UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINJI inatangaza nafasi za MAFUNZO
YA UTENGENEZAJI WA MASHINE ZA KUTOTOLEA VIFARANGA WA KUKU.
Mashine
zitakazo fundishwa kutengeneza ni INCUBATOR ( MANUAL &
AUTOMATIC) ZENYE UWEZO WA KUTUNZA JOTO KWA SAA 48 PAMOJA NA
KUTOTORESHA MAYAI KUANZIA 240 HADI 5000.
Vile vile yatatolewa mafunzo ya UTENGENEZAJI WA MAJIKO SANIFU NA NISHATI MBADALA.
ADA YA MAFUNZO :
Ada ya mafunzo haya ni SHILINGI ELFU ISHIRINI NA TANO TU. (Tshs.25,000/=)
TAREHE YA KUANZA KWA MAFUNZO
Mafunzo haya yatafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 01 SEPTEMBA 2014 hadi tarehe 05 SEPTEMBA 2014
FOMU ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO :
Fomu
za kujiunga na mafunzo haya zinapatikana ofisini kwetu kwa
gharama ya SHILINGI ELFU KUMI NA TANO TU ( Tshs.15,000/=).
MWISHO WA KUCHUKUA FOMU :
Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 28 AGOSTI 2014.
Ofisi zetu zinapatikana katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU.
JINSI YA KUFIKA OFISINI KWETU
Kufika
ofisini kwetu, panda daladala za UBUNGO- CHANGANYIKENI kisha
shuka kituo cha TAKWIMU halafu tembea hatua ishirini mbele
kisha tazama upande wako wa kulia utaona ofisi imeandikwa RAEFO
TANZANIA.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu 0784406508.
Kwa taarifa zaidi kuhusu mafunzo ya utengenezaji wa mashine za kutotolea vifaranga, tembelea :
Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
No comments:
Post a Comment