Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Mkuu wa Chuo cha Sebastian Kolowa Memorial University SEKOMU Askofu
Dr.Stephen Munga(kushoto)Makamu Mkuu wa Chuo cha SEKOMU Dr.Anneth
Munga(watatu kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa(kulia)
wakikata utepe kuzindua rasmi ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William
Mkapa wilayani Lushoto
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni muda mfupi
baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu chA Sebastian Kolowa Memorial
University mabapo alifungua ukumbi wa mihadhara na kuhutubia
wananchi.Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha SEKOMU Askofu Dr.Stephen Munga na
kulia ni makamu wa chuo Dr.Anneth Munga.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasililiza kwa makini wanafunzi kutoka
Irente school for the Blind wakati walipoimba shairi maalumu wakati wa
sherehe za ufunguzi wa ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa
katika chuo kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University SEKOMU
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanafunzi wa wageni waliohudhuria
sherehe ya ufunguzi wa ukumbi wa mihadhara wa Benjamin William Mkapa
uliofanyika katika chuo kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University
SEKOMU huko Lushoto Mkoani Tanga
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini
kuhakikisha kuwa wanashirikiana na Wananchi kuhakikisha kuwa ifikapo
Mwezi Novemba Mwaka huu, kila Shule ya Sekondari katika maeneo yao,
ina maabara kwa ajili ya masomo ya Sayansi.
Rais
Kikwete amesema hayo Mkoani Tanga katika nyakati tofauti Wilayani
Kilindi na Lushoto ambapo yuko katika ziara ya kikazi Mkoani Tanga tangu
tarehe 8 Julai hadi tarehe 12 Julai,2014.
"Nataka ifikapo Mwezi Novemba, Mwaka huu vyumba vya maabara viwe vimekamilika, tulipeana miaka miwili, imetimia" Rais
amesema na kuongeza kuwa lazima tusahihishe makosa tuliyofanywa ya
kutojenga maabara wakati tunajenga shule za sekondari nchini kote.
Mwaka
2006, Serikali ilihamasisha ujenzi wa Shule za Sekondari nchini kote na
muitikio ni mzuri, lakini hakukuwa na uhamasishaji wa kujenga maabara.
“Tumeamua kushughulikia suala la maabara ili kuongeza idadi ya wanafunzi
wa masomo ya Sayansi kote nchini." Rais amesisitiza.
Rais
amesema ameridhika na upanuzi wa Elimu katika ngazi za Msingi na
Sekondari kote nchini na Serikali inaendelea na hatua ya kutatua
changamoto za ubora wa Elimu, kuongeza Walimu, kuongeza Vitabu, ujenzi
wa Maabara na Nyumba za Walimu kote nchini.
Akihutubia
katika mkutano wa hadhara Wilayani Lushoto Rais ameahidi kuboresha na
kushughulikia suala la ujenzi wa barabara ya kwenda Bumbuli na zaidi
kuhakikisha anaweka barabara ya lami katika mji wa Lushoto na mji mdogo
wa Bumbuli.
Rais anaendelea na ziara Wilayani Lushoto na Mkinga ambapo anaendelea kuzindua miradi na kukagua miradi ya maendeleo.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Julai,2014
Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
No comments:
Post a Comment