Social Icons

Sunday, 22 June 2014

NEWS: RAIS WA CHUO CHA BUGANDO ALIYEPOTEA TOKA TAR 18 MWEZI HUU APATIKANA AKIWA KAPOTEZA FAHAMU MAENEO YA USAGARA

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 


Bw.Mussa Leonard Mdede Aliyesimama.

Rais wa chuo kikuu cha CUHAS (Bugando) na Mwenyekiti wa Shirikisho la wanafunzi vyuo vikuu nchini (TAHLISO), Bw.Mussa Leonard Mdede ameokotwa usiku huu  katika maeneo ya Usagara nje kidogo ya jiji la Mwanza, akiwa amepoteza fahamu (hajitambui)  lakini hana majeraha yoyote na amepelekwa katika hospitali ya rufaa Bugando kwa ajili ya vipimo na kupatiwa matibabu.Kwa sasa ameweza kuongea (japo kwa taabu) lakini hakumbuki chochote kilichotokea.

Bw.Mdede alitoweka ghafla siku ya jumatano tar.18 mwezi huu, saa kumi jioni,na haikuweza kufahamika mara moja yupo wapi, mpaka usiku huu taarifa za kupatikana kwake zilipotolewa.Taarifa hizi zimedhibitishwa na Waziri Mkuu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Bw.Benjamin Thomas. Taarifa zaidi juu ya hali ya Bw.Mdede zitazidi kutolewa kwa kadri zinavyopatikana.

 Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mwanza ameahidi kutoa taarifa leo.

SOURCE: Nicholaus Kilunga (mwandishi aliyepo mkoani Mwanza)

No comments: