Ofisa Masoko Mwandamizi Access Bank, Muganyizi Bisheko (kulia)
akimkabidhi moja ya kompyuta Mkuu wa Shule ya Sekondari Azania, Mwl.
Benald Ngonzie (kushoto), wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni wanafunzi
wa shule hiyo. Benki hiyo jana ilitoa msaada wa kompyuta 10 kwa shule
hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
Ofisa Masoko Mwandamizi Access Bank, Muganyizi Bisheko (kulia)
akimkabidhi moja ya kompyuta kwa wanafunzi waliowawakilisha wenzao,
anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Shule hiyo, Mwl. Benald
Ngonzie. Benki hiyo jana ilitoa msaada wa kompyuta 10 kwa shule hiyo
zenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
Ofisa Masoko Mwandamizi Access Bank, Muganyizi Bisheko (kulia)
akimkabidhi moja ya kompyuta makamu wa rais wa shule ya sekondari ya
Azania, Johnson Kaaya, wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa shule
hiyo, Mwl. Benald Ngonzie. Benki hiyo jana ilitoa msaada wa kompyuta 10
kwa shule hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Azania, Mwl. Benald Ngonzie akiongea
na wanafunzi mara baada ya makabidhiano ya kompyuta kwa shule hiyo
iliyotolewa na Access Bank. Benki hiyo jana ilitoa msaada wa kompyuta
10 kwa shule hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
Ofisa Masoko Mwandamizi Access Bank, Muganyizi Bisheko akiongea na
vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi kompyuta kwa shule hiyo. Picha
zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Shule ya sekondari ya Azania inakabiliwa na uchakavu wa miundombinu
ikiwamo majengo na ubovu wa vyoo, hali inayohatarisha afya za wanafunzi
hao kutokana na kuwapo kwa majimaji anayoweza kuzalisha mbu waenezao
ugonjwa wa Malaria na Dengue.
Akizungumza jana baada ya kupokea msaada wa kompyuta 10 kutoka katika
benki ya Access, Makamu Mkuu wa shule hiyo Elizabeth Ngoda alisema
shule hiyo ni kongwe kwa sasa kutokana na kujengwa muda mrefu hivyo
inahitajika ukarabati wa kina.
"Shule ni kongwe na imezalisha viongozi mbalimbali na sasa imechakaa,
majengo yanahitajikukarabatiwa na vyoo havitoshi, lakini tunawashukuru
Access Bank kwa kutuletea kompyuta hizi, kwani tulikuwa na kompyuta 25
awali ambazo hazikukidhi mahitaji kutokana na kuwa na idadi kubwa ya
wanafunzi," alisema Ngoda na kubainisha kwamba shule ina wanafunzi 2000
na wafanyakazi 115.
Ngoda alitoa wito kwa wadau wengine pamoja na wanafunzi waliowahi
kusoma katika shule hiyo,kujitolea kwa hali na mali ili kuirudisha
Azania katika hali nzuri ya kimazingira.
Makamu wa rais wa shule hiyo Johnson Kaaya aliwashukuru wadau hao
huku akitoa wito kwa makampuni mengine kuchangia katika kurekebisha
kasoro kadhaa zilizopo shuleni hapo hasa miundombinu.
"Tunaahidi kuzitumia kompyuta hizi katika kuleta ufanisi na si
vinginevyo, tunaomba hii iwe chachu kwa makampuni mengine kusaidia zaidi
kwani changamoto kubwa hapa shuleni kwetu ni uchakavu wa majengo,
hatuna viti, vyoo vibovu na pia tunapata taabu kipindi cha joto kwani
hakuna feni," alisema Kaaya.
Naye Ofisa Masoko Mwandamizi wa Access Bank, Muganyizi Bisheko
alisema msaada huo ni katika mwendelezo wa mchakato wa kusaidia sekta ya
elimu nchini hasa katika upane wa teknolojia ya abari na mawasiliano
ambayo imeonekana kuwa kikwazo kikubwa katika utafutaji wa ajira kwa
vijana ambao humaliza shule bila kuwa na utaalamu wa kompyuta.
"Tunaamini kupitia kompyuta hizi wanafunzi wataweza kujifunza
programu mbalimbali ambazo zitawasaidia katika kukuza elimu yao hapa
shuleni na katika maisha yao," alisema Bisheko.
No comments:
Post a Comment