Na Joseph Ngilisho, ARUSHA
SIRI nzito ya mauaji ya kinyama ya mwanafunzi wa Chuo cha Savanna Bridge
cha jijini Arusha, Winfrida Akunay (18) aliyechomwa kisu mara sita eneo
la shingo na kifua mbele ya baba yake mzazi imegundulika, Amani
linakupatia.
Winfrida Akunay (18) enzi za uhai wake.
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani, mtuhumiwa wa mauaji hayo, Robert Isaac
(22) alitimiza ukatili huo nyumbani kwa baba wa marehemu Majengo Juu
jijini hapa, Machi 25, mwaka huu, saa 2:12 usiku.
Ishu kubwa iliyojitokeza ni wivu wa mapenzi ambapo mgogoro mzito uliibuka kwa wawili hao.
Gazeti hili lilifuatilia kwa makini sakata la mauji hayo na kufanikiwa
kupata waraka wa siri ulioandikwa na mtuhumiwa huyo ambapo sehemu ya
waraka ilisema:
"Nakupa wiki moja ya kufikiria, kama utaendelea na msimamo wako wa
kutokuwa na mimi nitakuua kwa mikono yangu mwenyewe na mimi kujiua."
Mwenyekiti wa Mtaa wa Remtula, Majengo alisema baada ya mauaji hayo
kesho yake walikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa eneo la Ngusero alipokuwa
akiiishi na mjomba wake na kufanya upekuzi chumbani ambapo walikuta
karatasi iliyoandikwa:
"Mimi Robert Isaac nikiwa na akili timamu, nilikuwa na marehemu Winfrida
kama wachumba kwa muda wa miaka miwili iliyopita, tuliahidiana kuoana
baada ya kula yamini ya damu, lakini ilipofika mwezi wa pili, mwaka huu,
marehemu alinikataa, lakini mwezi wa tatu tulifanikiwa kurejesha
mahusiano mara tatu.”
GPL
SIKILIZA TONE RADIO HAPA LIVE
Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
No comments:
Post a Comment