Social Icons

Thursday, 6 March 2014

SHULE BINAFSI NA MCHANGO WAKE WA PEKEE KATIKA SEKTA YA ELIMU HAPA NCHINI
 SHULE binasi zina mchango wa pekee katika sekta ya elimu hapanchini,  kwa kutambua wingi wa watoto na ufinyu wa nafasi za shule za serikali


zilizopo.

Hiyo imefanya serikali kuchagua wale wenye uelewa wa juu pekee
kujiunga na shuleza elimu ya juu, huku wale ambao pengine kwa bahati  mbaya wamekwama kufikia alama zilizowekwa na serikali, wakiokolewa na


shule binafsi.

Hii imesaidia idadi kubwa ya watoto nchini kupata elimu ya sekondari
tofauti na miaka ya nyuma ambapo watoto wengi waliokuwa wakifeli na
kukosa shule basi huishia nyumba.

Shule za Filbert Bayi, nazo ni miongoni mwa shule binafsi zilizokuwa
na mchango wa pekee, hususani katika elimu ya sekondari.

Miaka  tangu kuanzishwa kwa shule ya Sekondari Filbert Bayi, na miaka
sita ya mahafali ya kidato cha nne, imeweza kuonyesha maajabu ya aina
yake kwa kufuta kabisa daraja sifuri.

Shule ilianza ikiwa na wanafunzi 28 na hadi sasa wamefikia 380, na
Mkurugenzi wa shule hizo Anna Bayi anasema wamefikia idadi hiyo kwa
sababu  ya kuchagua watoto wanaokidhi viwangovilivyowekwa na shule.

"Tungekuwa tunachukua watoto wa kila aina, basi nadhani idadi ingekuwa
kubwa zaid, lakini kwanza hatupokei watoto we na wenye utovu wa
nidhamu na wenye uelewa  wa hali ya chini.

Anasema ingawa wanachangamoto  ya kuachiwa watoto wasio na uelewa
sana, kwa kuzingatia wote wanaofanya vizuri kuchukuliwa shule za
serikali, lakini bado wameweza kutoa watoto bora kielimu.

Hata  hivyo, nao huwachuja na kupata wenye uelewa wastani, na tangu
wameanza kufanyamitihani yakidatocha nne hawajawahi kupata daraja
sifuri.

"Tulianza kwa kupata dara la nne, ambapo walikuwa wachache sana,na
tulishuka hadi akabaki mmoja, na mwaka jana hatukupata daraja la nne,
na badala yake daraja moja na mbili ndio walikuwa wengi huku daraja la
tatu wakiwa wachachekabisa,"anabainisha.

Kutokana na matokeo hayo, shule ya sekondari Filbert Bayi iliyoko
Kibaha mkoani Pwani, imefanikiwa kushika nafasi ya sita kimkoa, kati
ya shule 105,na nafasi ya 71 kitaifa kati ya shule zaidi ya 3000 na
nafasi ya nne kiwilaya.

Pamoja na mafanikio hayo, lakini shule hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo kubwa ya kunyoosha maadili ya watotona hatimaye
kuwa wamoja.

"Kila mmoja anatoka kwenye mazingira na makuzi ya aina yake, na
anapofika hapa tunataka awe na tabia zenye kupendeza machoni mwa watu,
na kama unavyojua watoto wengi wa sekondari wanafika wakiwa na umri wa
kufanya matendo ya kipumbavu, basi tunahangaika nao hadi  wanakaa
sawa,"anaongeza.

Anasema ingawa yeye ni mkurugenzi lakini kuna wakati anasimama kama
mama, akielewa fika wazazi wengi siku hizi malezi yao hayasimama sawa
kimaadili.

Anna anasema wazazi wengi hawakai na watoto wao na wengi hawajui pia
tabia za watoto hao, kitu ambacho si sawa hasa nyakati hizi za sayansi
na teknolojia.

"Unaweza ukamuita mzazi aje kusikiliza matatizo ya mwanaye anayevaa
nguo fupi ama mlegezo, na anapokuja anakuwa kavaa kama mwanaye, kiasi
hata maneno ya kumkanya mtoto unakosa,"anabainisha.

Ili kuwafanya wanafunzi wabobee katika masomo na si kitu kingine,
anasema wameweka mitihani ya majaribio mara mbili kwa wiki, na hivyo
siku za mapumziko huzitumia kuajindaa na mitihani.

Anaongeza kuwa mazingira ya shule yamewekwa kirafiki na wanafunzi, na
ni lazima mtoto akutwe nakitabu cha kujisomea wakati wote awapo eneo
la shule.

Licha ya kusimama kitaaluma, pia shule hizo huongoza katika sekta ya
michezo pamoja na stadi nyingine za maisha.

Anasema huwapa watoto kazi za mikono kwa ajili ya ujasiriamali, ambapo
kuna wanaofuga kuku wa mayai na nyama, walima bustani za mbogamboga,  wanaofundishwa upambaji pamoja na mapishi.Mkurugenzi huyo anasema kunapokuwa na shughuli yoyote shuleni
inayohitaji kupamba maeneo, basi wanafunzi ndio hufanya kazi hiyo,
kwa matokeo ya ufanisi mkubwa.


"Tunamjenga mtoto kuwa mbunifu katika maisha na anapotoka hapa,
anakuwa na shughuli za kufanya huko nyumbani, ni elimu ambayo hata
wenyewe wanaifurahia sana nainawajenga kiakili pia,"anaongeza.

Anaongeza kuwa suala la kufuta daraja sifuri si dogo hasa kwa shule
ambayo inachukua watoto wenye uelewa wa chini.

Hivyo, ili kuzidi kuwapa moyo walimu, hutoamotisha ya  sh. milioni
mojakwa kila mwalimu wa somo lililofanya vizuri.

"Nina walimu 10 wanaofundisha kidato cha nne, ambao wote kwa mwaka huu
wanastahili sh.milioni moja moja, na nimewaandaliwa hafla maalum ya
kuwakabidhi vitita vyao, hii italeta faraja na motisha kwao ili wazidi
kufundisha kwa juhudi,"anafafanua.

Anasema kifuta jasho hicho huwa hakitoki katika mitihani ya taifa tu,
bali hata mitihani ya mwisho wa mwaka kwa walimu ambao masomo yao
yatafanya vizuri.

Pia anasema ili mtoto aweze kufanya vizuri anastahili kuwa msafi yeye
pamoja na eneo linalomzunguka, hivyo wameandaa vikombe ya usafi
ambavyo hushindaniwa kila mwezi.

"Tunashindanisha usafi wa kuanzia vyumbani, madarasani ndani na
kuzunguka nje na mavazi kwa ujumla, na bweni litakalopata kikombe,
linaandaliwa hafla ndogo yenye vitafunwa vya sambusa na soda,"anasema.

Kuna watoto ambao kwa ujumla hawapendi kuandika, na wanapogundulika,
Anna anasema hupewa adhabu ya kali za kuwajenga, zikihusisha kuandika
notisi nyingi zaidi kuliko alizokwepa.

"Katika somo la hesabu nakoni shida, hivyo tunawapa watoto wakariri
tebo ya kuzidisha na tunaandaa mashindano kabisa, kwa wale wasiofanya
vizuri kwa kweli tunakuwa wakali sana,"anasema.

Hata wanapokuwa likizo majumbani, pia hupewa kazi za shule za kwenda
kufanya na pindi mtoto anaporudi shuleni bila kukamilisha hurudishwa
na mzazi.

Kwenye changamoto za kiuendeshaji anasema kwa kiasi kikubwa zinatokana
na serikali, ambayo imekuwa ikiwarundikia kodi na michango ya kila
aina hata kusababisha shule nyingine kufungwa.

"Serikali  haituoni sisi kama wasaidizi katika kuinua sekta ya elimu
hapa nchini balitunaonekana tofauti, tunabambikiwa ada nyingi kweli,
wanataka hicho kidogo tunachopata tugawane nusu kwa nusu.

"Mfano mdogo ni hapa kwangu, ada sh. milioni mbili tu, lakini hiyo
hiyo mtoto ale vizuri na apate huduma zote muhimu, huku kodi ya
ukaguzi wa elimu, sh. 2000 kila mtoto ikinisubiri, bado Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Zimamoto, Usalama kazini, mitihani na majengo,
wakati huo huo ukichunguza kodi zote zinafanana matumizi
yake,"anaongeza.

Anasema kwa wao waliochukua mikopo ya kujenga shulekuna muda
wanakwama, na pia serikali imekuwa ikiongeza gharama kila wakati bila
kujali na wala kushirikishwa wakati mwingine.

Anaongeza kuwa kama wangeshirikishwa katika masuala mengi basi elimu
ya Tanzania ingefika mbali mno.

Na hilo pia linagusa hata katika ratiba zamitihani ambayo serikali
imetoa amri na shulebinafsi kufanya, na wakati mwingine husababisha
ratiba kuingiliana na za shule husika, na yoteni kutokana na
ushirikishwaji haba.

Anna anabainisha kuwa wanashindwa kuchangia elimu elimu ya serikali,
kama vile kusaidia vitabu katika shule za kata, madawati na msaada
mwingine kwa sababu wanabanwa na kodi.

Anasema kodi hizo wakati mwingine zinasababisha mmiliki wa shule
asitengeneze watoto wanaotakiwa kuwa katika ulimwengu wa maendeleo.

Akirudi kwa upande wa mikakati ya shule, anasema kuanzia mwaka jana
wameanza kuchukua watoto wa kikepekee, ili baadaye shule hiyo iwe kwa
ajili ya wasichana tu.

Anasema hata ukifika sasa shuleni, utaona wavulana ni wachache, na
lengo ni kuwainua wanawake hapo baadaye waje kuongoza sekta
mbalimbali.

"Kusimamia watoto wa kike ni rahisi zaidi kuliko wanaume, hivyo
tunataka kutumia muda mzuri kuwaandaa na baadaye tuje kujivunia kutoa
viongozi na hata Rais,"anasema.

Shule za msingi za Filbert Bayi nazo zimekuwa zikifanya vizuri, na
anasema hadi sasa zina wanafunzi 860 kampasi zote.

Anna anasema amendeleo ya shule hizo ni mazuri na ufaulu wao kwa
darasa la saba ni wa asilimia  100.

"Hata darasa la nne nao wamefaulu vizuri tu na pia kuna motisha kwa
walimu wa shule za msingi wanaofanya vizuri, hatutoi motisha kwa shule
za sekondari tu,"anaongeza.

Kwa sasa wanajenga uwanja mkubwa wa michezo, ambao utakuwa na daraja
la kimataifa, na ni matumaini yake kwamba michezo mingi itakayofanyika
mkoani wa Pwani, itatumia uwanja huo.

No comments: